Shanghai ni mji mkubwa kuliko yote nchini China wenye wakazi milioni 14 ambao pamoja na rundiko la jiji ni takriban milioni 20. Iko mdomoni mwa mto Yangtze.

Shanghai

Katika historia ilikuwa bandari muhimu. Wakati wa karne ya 19 China ililazimishwa na Uingereza kukubali Shanghai iwe bandari kwa meli za nje na biashara ya kimataifa. Kwa njia hiyo ilikuwa geti la China kwa dunia ikaanza kukua sana. Waingereza, Wajapani na Wamarekani wote walipewa maeneo yao walipokuwa na mamlaka. Maeneo hayo yote yaliunganishwa kama mtaa wa kimataifa wa Shanghai.

Tangu mwaka 1949 mji uliunganishwa baada ya mapinduzi ya kikomunisti yaliyotangaza mwisho wa mtaa wa kimataifa. Maendeleo ya mji yalikwama hadi miaka ya 1980 China ilipoamua kujiunga tena na uchumi wa kimataifa na Shanghai ikawa kitovu cha biashara hii na kuzidi kukua haraka.

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Shanghai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.