Paa-chonge
Paa-chonge wa Afrika katika Museum of Natural History, London
Paa-chonge wa Afrika katika Museum of Natural History, London
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Tragulidae (Wanyama walio na mnasaba na paa-chonge)
Milne-Edwards, 1864
Ngazi za chini

Jenasi 3:

Paa-chonge ni wanyama wadogo wa familia Tragulidae katika oda Artiodactyla. Spishi kadhaa za paa-chonge ni wanyama wadogo kabisa miongoni mwa oda hii. Wapewa jina lao kwa sababu wana chonge zilizorefuka. Zile za madume ni ndefu sana na zinachomoza nje kutoka kila upande wa utaya wa juu na hutumika wakati wa mapigano. Paa-chonge hawana pembe lakini wana miguu mifupi na myembamba yenye vidole vinne. Manyoya yao yana rangi ya kahawa au kahawianyekundu na tumbo ni jeupe. Wana michirizi na madoa meupe au njano isipokuwa spishi za jenasi Tragulus. Spishi moja inatokea misitu ya mvua ya Afrika lakini spishi nyingine zinatokea misitu ya Asia ya Kusini na ya Kusini-Mashariki. Hula nyasi na majani, lakini paa-chonge wa Afrika hula wadudu, kaa na mizoga ya wanyama na samaki pia.

Spishi ya Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paa-chonge kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu "Paa-chonge" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili fanged deer kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni paa-chonge.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.