Panya-miti
Panya-miti kinyago (Graphiurus ocularis)
Panya-miti kinyago (Graphiurus ocularis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Sciuromorpha (Wanyama kama kindi)
Familia: Gliridae
Muirhead, 1819
Ngazi za chini

Jenasi 9, spishi 29:

Panya-miti ni wanyama wadogo wa familia Gliridae. Spishi nyingi hupanda miti na huishi katika matundu ya mti au matago ya ndege. Wanyama hawa wanafanana na kindi wadogo. Urefu wa mwili wao ni kutoka mnamo sm 8 hadi sm 20 na wana mkia wenye urefu karibu na mwili. Rangi yao ni kahawia, kijivu au nyeusi na chini nyeupe kwa kawaida. Spishi nyingine zina mabaka. Hula beri, matunda na makokwa hasa lakini maua, majani, gamba la mti, wadudu na mayai pia. Jike huzaa hadi zaidi ya watoto 10.

Panya-miti wa kulika alikuwa huliwa sana na Warumi wa kale. Siku hizi bado huliwa huko Slovenia

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Ulaya na Asia

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri