Patasi
Patasi ni zana ya metali inayotumiwa na seremala au mwashi kukata, kupunguza au kuchonga ubao, jiwe au metali. Metali yake kwa kawaida ni chuma au feleji. Umbo lake ni kama nondo yenye makali upande moja na sehemu ya kugongwa kwa nyundo upande mwingine.
Patasi kwa kazi za ubao hupatikana kwa upana na uzito tofauti, kuanzia patasi kubwa ya kupunguza vipande vikubwa hadi patasi ndogo kwa kazi ndogondogo.
Patasi kwa kazi ya kuchonga mawe au mwamba ni nzito zaidi.
Picha
hariri-
Mwashi akitumia patasi kuandaa jiwe la kaburi
-
Mwashi akitumia patasi kutengeneza mpira wa mawe
-
Kuandaa nafasi ya bawaba ya mlango kwa patasi ya ubao
-
Seremala anakata kiungo cha umana kwa patasi ya ubao