Open main menu

Chuma cha pua

(Elekezwa kutoka Feleji)
Daraja la reli nchini Argentina ilitengenezwa kwa kutumia feleji
Mnara wa Eiffel mwenye kimo cha mita 300 ilikuwa jengo kubwa la dunia; imetengenzewa kwa chumapua tu
Chumapua moto katika hali ya kiowevu yamwagwa kutoka jiko lake


Chuma cha pua (pia: chumapua, feleji) ni aloi wa chuma pamoja na gredi mbalimbali za kaboni ambayo imekuwa uti wa mgongo wa mapinduzi ya viwandani. Hadi leo ni msingi wa mashine na vifaa vingi pia silaha zinazounda uwezo wa kijeshi wa mataifa. Pia ujenzi wa kisasa hauwezekani bila chuma cha pua.

Chuma cha pua ni ngumu kushinda chuma tupu isiyo na kaboni. Siku hizi kuna pia aloy za chumapua ambamo dutu tofauti na kaboni hutumiwa.

Historia ya chumapuaEdit

Kutengenezwa kwa chumapua kulikuwa sanaa ya pekee kwa karne nyingi. Silaha kama panga za chumapua zilikuwa bora kushinda panga za chuma cha kawaida. Vilevile vifaa kama visu hata jembe vilidumu kama vilitengenezwa kwa chumapua. Wahunzi walipeana mbinu za kutengeneza chumapua kama siri, kwa mfano kati ya wahunzi wa kijadi wa Wahaya wa maeneo karibu na Ziwa Viktoria[1].

Tangu 1610 viwanda katika Uingereza vilianza kutengeneza chumapua kwa vingi ikaboreshwa katika miaka 100 iliyofuata. Mbinu huo ulikuwa msingi wa maendleo ya Uingereza juu ya mataifa mengi mengine katika mapinduzi wa viwandani. Mashine zote zilitengenezwa kwa chumapua.

Mnara wa Eiffel ulikuwa jengo kubwa la kwanza lililoundwa na chumapua pekee. Meli za chumapua zilichukua nafasi ya jahazi za awali za ubao.

Tabia za chumapuaEdit

Tabia za chumapua hutegemea na kiasi cha kaboni ndani yake. Kiasi kikubwa cha kaboni husabibisha aloi kuwa ngumu zaidi lakini inavunjika kirahisi pia. Kiasi kidogo cha kaboni husababisha chumapua kuwa laini zaidi lakini inanapukia zaidi.

Chumapua cha kawaida huhitaji kiinga dhidi ya kutu kama vile rangi au kupakwa kwa zinki.

Nyongeza za kromi zababisha chumapua kutoshika kutu. Hivyo vifaa vya chakula kama vile uma, visu au vijiko hutengenezwa na aloi hiyo, pia vifaa vya madaktari kama vile visu vya upasuaji.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Peter Schmidt and Donald H. Avery: Complex Iron Smelting and Prehistoric Culture in Tanzania, Science Journal, New Series, Vol. 201, No. 4361 (Sep. 22, 1978), pp. 1085-1089 online hapa