Jongoo Miguu-michache
(Elekezwa kutoka Pauropoda)
Jongoo miguu-michache | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Spishi isiyotambuliwa ya Pauropoda
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Familia: |
Majongoo miguu-michache ni aina za arithropodi wadogo katika ngeli Pauropoda ya nusufaila Myriopoda. Wana mnasaba na majongoo ya kawaida lakini wana urefu mfupi (mm 0.5-2) na miguu michache kuliko hawa (jozi 9-11 katika wanyama wazima). Vipapasio vyao vina vitawi. Hawana macho wala moyo. Huonekana katika udongo na inawezekana kama hula kuvu na dutu ya viumbehai.
Picha
hariri-
Jongoo miguu-michache wa Huxley