Port Bell

Port Bell ni mji mdogo karibu na Kampala/ Uganda ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Jina la mji limetokana na Sir Hesketh Bell aliyekuwa kamishna (gavana) Mwingereza huko Uganda kuanzia mw. 1905-1909.

Mahali pa Port Bell katika Uganda

Port Bell ni bandari kwa ajili ya Kampala. Feri zinatoka kwenda Jinja, Kisumu na Mwanza.

Kuna viwanda kadhaa kama vile Kiwanda cha Bia cha Uganda Breweries; bia ya Bell Lager inatengenezwa hapa. Kuna pia kiwanda cha pombe kali aina ya Waragi na kiwanda cha chai.