Porto Novo
Porto Novo (Kireno kwa: "Bandari mpya" - inaitwa na wenyeji pia Hogbonou na Adjache) ni mji mkuu rasmi wa Benin. Ni mji wa bandari kwenye kidaka cha Atlantiki.
Jiji la Porto Novo | |
Nchi | Benin |
---|
Mwaka 2002 Porto Novo ilikuwa na wakazi 223,552 (sensa 2002) na mji wa pili katika Benin. Hapa ni ikulu ya rais na makao ya bunge lakini wizara nyingi zina ofisi zao mjini Cotonou.
Historia
haririJina la kihistoria ni Ajache. Kwa jina hili mji ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Aja. Wareno walijenga kituo cha biashara ya watumwa wakaiita "Porto Novo - bandari mpya". Mwaka 1863 ufalme ulikubali ulinzi wa Ufaransa kwa hofu ya Waingerezea. 1883 eneo lake likawa sehemu ya koloni ya Kifaransa ya Dahomey na mwaka 1900 mji mkuuw a koloni yote.
Wafalme wa Porto Novo waliendelea kuwa na makao mjini hadi kifo cha mfalme wa mwisho Alohinto Gbeffa mwaka 1976.
Tangu mwisho wa utumwa huko Brazil Waafrika wa Brazil walirudi wakifika Porto Novo na kukaa hapa. Hivyo athira za Brazil zimeonekana katika utamaduni wa mji, hasa katika ujenzi na chakula.
Viungo vya Nje
hariri- Official Republic of Benin tourism site for Porto-Novo Ilihifadhiwa 9 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine.
- Official Benin government website information about Porto-Novo Ilihifadhiwa 5 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- porto-novo.biz Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Images of the Central Mosque of Porto-Novo Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Adjogan Ilihifadhiwa 4 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.