Mdudu Mkia-sahili
(Elekezwa kutoka Protura)
Mdudu mkia-sahili | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu mkia-sahili (Acerentomon sp.)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Oda na familia: |
Wadudu mkia-sahili ni wadudu wadogo bila mabawa wa nusungeli Protura (ngeli kufuatana na wataalamu wengi) katika nusufaila Hexapoda wasio na serki (cerci). Wana kiwiliwili kilichorefuka chenye urefu wa chini ya mm 2. Hawana macho wala vipapasio na wanakosa hata pigmenti na kwa hivyo wana rangi ya nyeupe au hudhurungi. Hubeba jozi ya kwanza ya miguu juu na kuitumia kama vipapasio. Spishi kadhaa zina spirakulo (spiracle) na trakea (trachea), lakini spishi nyingi hubadilisha gesi kwa njia ya ueneaji. Wadudu hawa wanatokea katika ardhi, chini ya mawe na nyuma ya gome la miti. Wakifugwa hula matitiri waliokufa, kuvu-mizizi na unga wa uyoga na msituni hula yumkini kuvu na maada ya mimea iliyokufa.
Picha
hariri-
Acerentomon sp.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mkia-sahili kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |