RETScreen
Programu ya Usimamizi wa Nishati Safi ya RETScreen (kwa kawaida iliyofupishwa kuwa RETScreen) ni kifurushi cha programu kilichotengenezwa na Serikali ya Kanada. RETScreen Expert iliangaziwa mwaka 2016 katika Clean Energy Ministerial iliyofanyika San Francisco.[1] Programu inapatikana katika lugha 36, ikiwa ni pamoja na Kiswahili.
RetScreen Expert ni toleo la sasa la programu na lilitolewa kwa umma mnano Septemba 19, 2016. Programu hii inaruhusu utambulisho, utathmini na uboreshaji kamili wa uwezekano wa kiufundi na wa kifedha wa nishati mbadala na miradi inayotumia nishati vizuri; ikijumuisha upimaji na uthibitishaji wa utendaji halisi wa vituo na utambulisho wa nafasi za kuokoa/uzalishaji nishati.[2] Hali ya mtazamaji" katika RETScreen Expert ni ya bila malipo na inaruhusu ufikiaji wa vitendaji vya programu. Hata hivyo, tofauti na matoleo ya zamani ya RETScreen,, "Hali mpya ya kitaalamu" (ambayo inaruhusu watumiaji kuhifadhi, kuchapisha, nk.) sasa inapatikana kwa msingi wa usajili wa kila mwaka.
RETScreen Suite, ikijumuisha RETScreen 4 na RETScreen Plus, ni toleo la awali la programu ya RETScreen. RETScreen Suite inajumuisha uwezo wa kuchambua uzajilishaji mbadala na wa nje ya gridi wa nishati.
Tofauti na RETScreen Suite, RETScreen Expert ni jukwaa moja lililojumuishwa la programu; hutumia chapa asili ya kina na ya jumla kwa kutathmini miradi; na inajumuisha uwezo wa kuchambua uwekezaji. RETScreen Expert hujumuisha hifadhidata kadhaa ili kumsaidia mtumiaji, pamoja na hifadhidata ya kimataifa ya hali ya hewa kutoka vituo 6,700 vya ardhini na data ya setilaiti ya NASA; hifadhidata ya vigezo, hifadhidata ya fedha, hifadhidata ya mradi, hifadhidata ya masuala ya maji na hifadhidata ya bidhaa.[3] Programu hii ina nyenzo nyingi za mafunzo, ikijumuisha kitabu pepe.[4]
Historia
haririToleo la kwanza la RETScren lilitolewa tarehe 30 Aprili, 1998. Toleo la 4 la RETScreen lilizinduliwa terehe 11 Disemba, 2007 kule Bali, Indonesia na Waziri wa Mazingira ya Kanada.[5] RETScreen Plus iliyotolewa mwaka wa 2011.[6] RETScreen Suite (ikijumuisha RETScreen 4 na RETScreen Plus ikiwa na maboresho mengi ya ziada), ilitolewa mwaka wa 2012.[7] RETScreen Expert ilitolewa kwa umma tarehe 19 September, 2016.[8]
Mahitaji ya programu
haririProgramu hiyo inahitaji Microsoft® Windows 7 SP1, Windows 8.1 au Windows 10; na Microsoft® .NET Framework 4.7 au ya juu zaidi.[9] Inawezekana kwa programu hiyo kufanya kazi kwa kompyuta za Apple Macintosh ikitumia Parallels au VirtualBox ya Mac.[10]
Washirika
haririRETScreen inasimamiwa chini ya uongozi na msaada wa kifedha unaoendelea wa Kituo cha Utafiti cha CanmetENERGY Varennes cha Rasilimali za Asili za Kanada, idara ya Serikali ya Kanada. Timu kuu[11] hushirikiana na mashirika mengine ya serikali na ya kimataifa, na msaada wa kitaalamu kutoka kwa mtandao mkubwa wa wataalamu kutoka kwa viwanda, serikali na shule.[12] Washirika wakuu ni pamoja na Langley Research Center ya NASA,[13] Renewable Energy and Energy Efficiency Partnership (REEEP),[14] Independent Electricity System Operator (IESO),[15] Kitengo chaNishati cha UNEP cha Idara ya Teknolojia, Viwanda na Uchumi,[16] Global Environment Facility (GEF),[17] Mchango wa Kupunguza Kaboni wa World Bank,[18] na Mpango wa Nishati Endelevu wa Chuo kikuu cha York.[19]
Mifano ya matumizi
haririKuanzia Februari 2018, programu ya RETScreen ilikuwa na watumiaji zaidi ya 575,000 katika kila nchi na himaya.[20]
Utafiti huru wa athari[21] ilikadiria kwamba kufikia mwaka wa 2013, matumizi ya programu ya RETScreen yaliwajibika duniani kote, kwa zaidi ya dola bilioni 8 katika kuokoa gharama ya muamala kwa watumiaji, MT 20 kwa mwaka wa upunguzaji wa uzalishaji wa gesi, na angalau imewezesha GW 24 ya uwezo wa nishati safi iliyowekwa.
RETScreen hutumika sana ili kuwezesha na kutekeleza miradi safi ya nishati. Kwa mfano, RETScreen imetumika:
- kuimarisha Empire State Building na hatua za ufanisi wa nishati[22]
- katika vituo vya utengenezaji vya 3M Canada[23]
- kwa kiasi kikubwa na sekta ya upepo ya Irish ili kuchambua miradi mpya ya uwezekano[24]
- kufuatilia utendaji wa mamia ya shule kule Ontario[25]
- na programu iliyochanganywa ya joto na nishati ya Manitoba Hydro (uboreshaji wa nishati) ili kuchunguza programu za mradi [26][27]
- kusimamia nishati kwenye chuo kikuu na chuo cha elimu[28]
- katika uchunguzi wa miaka mingi na kutathmini utendaji wa photovoltaic huko Toronto, Kanada[29][30]
- kuchambua upashaji joto hewa kwa kutumia jua katika Jeshi la Marekani[31]
- kwa vituo vya manispaa, ikijumuisha kutambua nafasi za ufanisi wa kuongezea vitu vya kuboresha nishati katika manispaa mbalimbali za Ontario[32][33]
Mkusanyiko mkubwa wa makala yanayoonyesha jinsi RETScreen imetumiwa katika muktadha tofauti, unapatikana kwenye ukurasa wa LinkedIn wa RETScreen.[34]
RETScreen pia hutumiwa kama chombo cha kufundisha na utafiti kwa zaidi ya vyuo vikuu na vyuo vya mseto 1,100 duniani kote, na mara nyingi hutajwa katika fasihi za kitaaluma.[35] Mifano ya matumizi ya RETScreen katika masomo inaweza kupatikana chini ya "Machapisho na Ripoti" na sehemu za "Mtalaa wa Chuo Kikuu na Chuo cha Elimu" za jarida la RETScreen, linalopatikana kwa njia ya mwongozo wa Mtumiaji kwenye programu iliyopakuliwa.
Matumizi ya RETScreen imeamurishwa au kupendekezwa na mipango ya motisha ya nishati katika ngazi zote za serikali duniani kote, ikijumuisha UNFCCC na EU; Kanada, New Zealand na Uingereza; majimbo mengi ya Amerika na mikoa ya; miji na manispaa ya Kanada; na matumizi.[36] Warsha za mafunzo ya RETScreen ya kitaifa na kimkoa zimetekelezwa kwa ombi rasmi la Serikali za Chile,[37] Saudia,[38] na nchi 15 za Afrika Magharibi na Kati,[39] na Shirika la Nishati la Amerika ya Kilatino (OLADE).
Tuzo na utambuzi
haririMwaka wa 2010, RETScreen ya Kimataifa ilipewa tuzo ya Utumishi Bora wa Umma,[40] tuzo kubwa zaidi lililotolewa na serikali ya Kanada kwa watumishi wake wa umma.
RETScreen na timu ya RETScreen wamechaguliwa na kupokea tuzo zingine nyingi za kifahari ikijumuisha tuzo la Nishati mbadala ya Kimataifa ya Ernst & Young/Euromoney, Nishati ya Dunia (Tuzo la Taifa la Kanada), na Medali ya Tuzo la Kipekee la GTEC.[41]
Mapitio
haririUchunguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati wa toleo beta la sehemu ya umeme ya programu hiyo ulielezea kama la "kuvutia sana".[42] Shirika la Mazingira la Ulaya linasema kwamba RETScreen "ni zana muhimu sana."[43] RETScreen pia imeitwa "mojawapo ya zana chache za programu, na bora zaidi inayopatikana kutathmini uchumi wa kuweka nishati mbadala" na "zana za kuimarisha...ushirikiano wa soko" katika nishati safi duniani kote.[21]
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Canada, Mexico and the United States Show Progress on North American Energy Collaboration". News.gc.ca. 2016-06-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-25. Iliwekwa mnamo 2016-10-20.
- ↑ Clean Energy Solutions Center. "Financial Analysis with RETScreen" (Video). Youtube.com. Iliwekwa mnamo 2016-10-20.
- ↑ "NASA - NASA Collaboration Benefits International Priorities of Energy Management". Nasa.gov. 2010-02-24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-07. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Clean Energy Project Analysis, RETScreen® Engineering & Cases Textbook: M154-13/2005E-PDF - Government of Canada Publications" (PDF). Publications.gc.ca. Iliwekwa mnamo 2016-02-24.
- ↑ "Archived - CANADA LAUNCHES CLEAN ENERGY SOFTWARE - Canada News Centre". News.gc.ca. 2007-12-11. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-12. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "RETScreen adds energy performance analysis module". REEEP.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International Newsletter - 2012-06-05: Major Upgrade to RETScreen Software". Web.archive.org. 2012-06-05. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-15. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International Newsletter - Coming Soon: RETScreen Expert Software". Web.archive.org. 2015-01-30. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-02. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "RETScreen, Natural Resources Canada". Nrcan.gc.ca. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - FAQ - Windows/Excel & other". Web.archive.org. 2015-04-24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-14. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International Core Team". Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-29. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Archived - RETScreen International Network of experts". Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-29. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "NASA - POWER". Nasa.gov. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Renewable Energy and Energy Efficiency Partnership (REEEP)". REEP.org. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "IESO". IESO.ca. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "About DTIE". Uneptie.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-08. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Global Environment Facility". Thegef.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-13. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Carbon Finance at the World Bank: Prototype Carbon Fund". Wbcarbonfinance.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-04-15. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Sustainable Energy Initiative". Yorku.ca. Iliwekwa mnamo 2018-02-13.
- ↑ "Archived - RETScreen International - RETScreen Software: Cumulative Growth of User Base". Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-20. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ 21.0 21.1 "Archived - RETScreen International: Results & impacts 1996-2012" (PDF). Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-09-26. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Energy Performance Contracting" (PDF). Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-05-11. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "3M Canada Deploys RETScreen Software".
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "Archived - RETScreen International - Wind Power and Biomass Heating Projects Seamus Hoyne, TEA and Tipperary Institute" (PDF). Web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-08-06. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "School Board Energy Managers Lead Way".
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "Bioenergy Optimization Program". Hydro.mb.ca. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Power Smart Bioenergy Optimization Program" (PDF). Web.archive.org. Juni 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-05-11. Iliwekwa mnamo 2016-10-24.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Universities and Colleges Reduce Carbon".
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "Solarcity Technology Assessment Partnership". Explace.on.ca. Juni 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Horse Palace Photovoltaic Pilot Project: Update Report" (PDF). Solarcitypartnership.ca. Januari 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-11-02. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "AN EVALUATION OF SOLAR AIR HEATING AT UNITED STATES AIR FORCE INSTALLATIONS". Dtic.mil. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-09. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Katelyn McFadyen and Cristina Guido - Municipal Energy Champions". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-08. Iliwekwa mnamo 2018-03-27.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "Internet Archive Wayback Machine". Web.archive.org. 2014-08-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-11. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
{{cite web}}
: Cite uses generic title (help) - ↑ "Archived - RETScreen International Newsletter". Web.archive.org. 2015-12-22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-12. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ Kwa mfano, utafutaji wa Google Scholar wa RETScreen mnamo tarehe 7 Februari 2018 ilionyesha matokeo 5,500.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Clean Energy Policy Toolkit". Web.archive.org. 2012-09-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-05. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - CER Chile Implements RETScreen Training Program". Web.archive.org. 2014-10-24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-14. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Saudi Arabia Builds Clean Energy Capacity". Web.archive.org. 2014-05-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-14. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Strengthening the Foundations of Clean Energy in West Africa". Web.archive.org. 2014-05-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-14. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Public Service Award of Excellence 2010" (PDF). Ottawacitizen.com. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Archived - RETScreen International - Awards". Web.archive.org. 2011-02-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-09. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.
- ↑ "Assessment Methods for Small-hydro Projects" (PDF). Ieahydro.org. Iliwekwa mnamo 2016-10-24.
- ↑ "RETScreen Clean Energy Project Analysis Software | Environmental software tools for accounting, carbon footprinting & sustainability performance". Environmenttools.co.uk. Iliwekwa mnamo 2016-07-15.