Rai Isoradio
Rai Isoradio ni kituo cha redio nchini Italia. Inalenga hasa waendesha magari ikirusha habari za hali ya barabara kuu za Italia (zinazojulikana kama Onda Verde) na ripoti za hali ya hewa, matangazo ya utumishi wa umma na mashirika mbalimbali ya serikali na ya umma, pamoja na habari za reli kutoka Shirika la Reli Italia FS, halafu taarifa za habari kutoka vituo vingine kama vile GR1, TG1 na TG3, na muziki.
Eneo lake | Italy - FM/Some Areas DAB, Hotbird satellite & Internet |
---|---|
Ilifika hewani | December 23, 1989 |
Aina ya programu | Highway advisory radio |
Mmiliki | RAI |
Webcast | Real Media |
Tovuti | https://www.raiplayradio.it/isoradio/ |
Kwa ushirikiano na mamlaka ya barabara kuu za Italia (Autostrade per l'Italia) Rai Isoradio inapelekwa kwenye barabara kuu zote za Italia (hasa kwa marudio ya MHz 103.3). Wakati wa saa za usiku (0:30-5:30, unaojulikana kama Isonotte), mtandao pia hubeba muziki wa Kiitalia usio na kikomo (unaokatizwa na taarifa za trafiki kila baada ya dakika 30).