Marudio (fizikia)
Marudio (ing. frequency, alama yake ni f) ni kipimo kichachosema ni mara ngapi tukio linatokea tena na tena kila baada ya kipindi fulani.
Kwa mfano ukikaa kando la bwawa au bahari penye mawimbi unaweza kuhesabu ni mawimbi mangapi yanayopita kwako katika dakika moja. Namba hii ni marudio ya mawimbi haya.
Kipimo cha SI kwa marudio ni Hezi (alama Hz).
Marudio katika mazingira yetu
haririVitu vingi katika dunia hutokea kwa marudio maalumu. Kutambua marudio ya mawimbi ya nuru, sauti, mawimbi ya sumakuumeme na kadhalika kumekuwa msingi kwa sehemu kubwa ya teknolojia tunayotumia, kuanzia redio, televisheni hadi simu na kompyuta.
Kwa hiyo marudio ni kipimo muhimu sana katika sayansi na teknolojia ya kisasa.
Marudio yanaweza kutajwa kwa matukio yote ambayo yanatokea mara kwa mara kufuatana na mfumo maalumu.
- Marudio ya badiliko la mchana na usiku ni
- Moyo wa binadamu ina mapigo 50-90 kila dakika hii inalingana na marudio ya 0.83–1.5 Hz).
- katika bendi au okestra wapiganaji wote wanahitaji kupanga ala zao kwa sauti ya marudio yaleyale, mara nyingi kwa 440 Hz.
- Sikio la kibinadamu hutambua sauti zenye marudio baina ya 20 Hz na 20.000 Hz, ilhali kiwango cha juu hupungua kuluingana na kuzidi kwa umri wa msikiliziaji.
- Jicho la kibinadamu huona nuru kati ya 400 THz na 750 THz (terahezi).
- Mawimbi ya sumakuumeme (ing. electromagnetic waves) hutumiwa kwa mawasiliano kwa redio au simu bila waya kuanzia 100 kHz na GHz kadhaa.
Marejeo
haririViungo vya Nje
hariri- Conversion: frequency to wavelength and back Archived 11 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- Conversion: period, cycle duration, periodic time to frequency
- Keyboard frequencies = naming of notes - The English and American system versus the German system
- Teaching resource for 14-16yrs on sound including frequency Archived 13 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- A simple tutorial on how to build a frequency meter Archived 18 Februari 2007 at the Wayback Machine.
- Frequency - diracdelta.co.uk Archived 15 Juni 2009 at the Wayback Machine. – JavaScript calculation.