Ram Prasad Bismil (11 Juni 189719 Disemba 1927) alikuwa mwanamapinduzi wa India aliyeshiriki katika njama maarufu za Mainpuri mwaka 1918, na Kakori mwaka 1925. Alikuwa mpiganiauhuru dhidi ya wakoloni wa serikali ya Uingereza, pia alikuwa mshairi mzalendo aliyeandika katika lugha ya Kiurdu akitumia lakabu ya Ram, Agyat na Bismil, lakini alijulikana zaidi kama "Bismil".

Ram Prasad Bismil

Bismil alikuwa mmoja wa waasisi wa chama cha kimapinduzi cha Hindustan Republican Association, alisifiwa zaidi na Bhagat Singh[1] kama mshairi gwiji wa Kiurdu na Kihindi ambaye alitafsiri vitabu katika lugha za Kiingereza na Kibengali.

Marejeo hariri

  1. Waraich, Malwinder Jit Singh (2007). Musings from the gallows : autobiography of Ram Prasad Bismil. Unistar Books, Ludhiana. p. 101. OCLC 180690320. 
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ram Prasad Bismil kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.