Mdudu Shingo-ngamia

(Elekezwa kutoka Raphidioptera)
Mdudu shingo-ngamia
Raphidia ophiopsis
Raphidia ophiopsis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Raphidioptera (Wadudu walio na shingo kama ngamia)
Handlirsch, 1908
Ngazi za chini

Familia 6

  • †Baissopteridae
  • †Chrysoraphidiidae
  • Inocelliidae
  • †Juroraphidiidae
  • †Mesoraphidiidae
  • Raphidiidae

Wadudu shingo-ngamia (kutoka kwa Kijerumani Kamelhalsfliegen) ni wadudu wakubwa kiasi wa oda Raphidioptera (raphio = sindano, ptera = mabawa) walio na shingo kama ngamia au kama nyoka (snakefly). Mabawa yao ni kama yale ya wadudu mabawa-vena, oda ambaye ndani yake wadudu hawa waliainishwa zamani. Wao ni wadudu mbuai na hula wadudu wengine wadogo, k.m. vidukari na matitiri. Hata lava hula wadudu wengine, mayai na lava hasa.

Wadudu hawa wanatokea katika misituni ya Nusudunia ya kaskazini. Kuna spishi tatu tu za wadudu shingo-ngamia katika Afrika kaskazini kwa Sahara. Hawatokei kusini kwa Sahara.

Spishi za Afrika hariri

  • Africoraphidia spilonota
  • Harraphidia harpyia
  • Mauroraphidia maghrebina

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Shingo-ngamia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hiyo kuhusu "Mdudu Shingo-ngamia" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.