Rejeta (kutoka Kiingereza radiator) ni kifaa kinachotoa joto kwenda mazingira yake. Rejeta hupokea joto ikiwa na uso mkubwa unaoachisha joto hilo katika mazingira yake penye joto kidogo.

Rejeta ya motokaa.
Injini ya pikipiki yenye pezi za kupoza.
Rejeta ya ukanzaji kwenye nyumba.

Rejeta kwenye motokaa

hariri

Motokaa zinazotumia injini ya mwako ndani huzalisha joto kubwa ndani ya injini. Joto hilo linapaswa kuondolewa nje. Kwa kusudi hilo kuna mabomba yenye maji au kiowevu kipozi kingine kinachopitishwa ndani ya injini ambako kipozi kinapokea joto. Kipozi husukumwa na pampu hadi rejeta kinapozunguka hadi kurudi kwenye injini. Ndani ya rejeta kiowevu kipozi kinapitishwa ndani ya mabomba membamba ambayo yanazungukwa na hewa ya nje. Hewa hiyo inasukumwa kupita kwenye rejeta kwa kasi kwa msaada wa parapela na mwendo wa gari. Hapa joto la kipozi ndani ya mabomba membamba linapotea katika hewa ya mazingira na kiowevu kilichopozwa kinarudishwa kwenda injini ambako kinapokea upya joto la mwako wa ndani.

Rejeta za hewa

hariri

Kuna pia rejeta ya hewa bila kiowevu kipozi. Hizi ni vifaa kama pezi za metali zinazoongoza uso wa kupoza. Rejeta ya hewa inapashwa moto pamoja na injini na kutoa joto kupitia uso wake. Rejeta za hewa hazina ufanisi sawa na rejeta za kiowevu. Siku hizi hazitumiwi tena kwa magari lakini zinapatikana kwa injini ndogo kama injini za pikipiki.

Rejeta kwenye mfumo wa ukanzaji

hariri

Katika ukanzaji wa nyumba (mfumo wa kupasha moto katika mazingira baridi) rejeta ni kifaa cha metali kinachotoa joto chumbani. Mara nyingi imeunganishwa kwa mabomba na jiko linalozalisha joto.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.