Parapela (kutoka Kilat. propellere = kusogeza mbele) ni jina la rafadha ikitumiwa kwenye eropleni.

Parapela (rafadha) ya eropleni

Parapela inatumia fizikia kama kila rafadha inasababisha tofauti ya kanieneo inayovuta ndege mbele.

Helikopta huwa na parapela mbili; parapela kubwa inavuta helikopta juu na parapela ndogo ya nyuma husaidia kulanga mwelekeo wake inapoenda.

Parapela za ndege hutengenezwa kwa kutumia ubao, plastiki na kwa mashine kubwa metali.