René Descartes
René Descartes (31 Machi 1596 – 1 Februari 1650) alikuwa mwanafalsafa, mwanahisabati na mwanafizikia mashuhuri katika Ufaransa.
Katika falsafa alijulikana kwa tamko lake "cogito ergo sum" (Kilatini: Ninafikiri hivyo niko; au: Nina hakika ya kwamba niko kwa sababu najikuta nikitafakari).
Alieleza nadharia yake katika kitabu "Discours de la méthode pour bien conduire sa raison et chercher la vérité dans les sciences" (tafsiri kamili: "Majadiliano juu ya mbinu jinsi gani kutumia akili vizuri na kutafuta ukweli katika sayansi").
Katika hisabati akumbukwa kama mwanzilishaji wa mfumo majira.
Athira yake ilikuwa kubwa kwa karne nyingi hata pale ambako matokeo ya nadharia zake yalifutwa baadaye.