Roland Brown
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania
Roland Brown alikuwa Mwingereza wa kwanza kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanganyika iliyokuja kuwa sehemu ya Tanzania baadaye.[1]
Maisha ya awali na taaluma
haririBrown alikuwa mkufunzi katika chuo cha Trinity College, Cambridge katika Chuo kikuu cha Cambridge, wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika; aliteuliwa kuwa mshauri mkuu wa Mwalimu Julius Nyerere.[2]
Tanzania
haririMwaka 1961 aliteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza baada ya uhuru wa Tanganyika.[3] Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoangusha utawala wa kisultani, Brown aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuandaa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.[4]
Mwaka 1965 alimaliza muda wake na nafasi yake ikachukuliwa na Mark Bomani.
Marejeo
hariri- ↑ "JOAN WICKEN". tzaffairs.org. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Charles Parkinson (22 Novemba 2007). Bills of Rights and Decolonization: The Emergence of Domestic Human Rights Instruments in Britain's Overseas Territories. Oxford University Press. ku. 231–. ISBN 978-0-19-923193-5.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ James Clagett Taylor (1963). The Political Development of Tanganyika. Stanford University Press. ku. 197–. ISBN 978-0-8047-0147-1.
- ↑ Godfrey Mwakikagile (2008). The Union of Tanganyika and Zanzibar: Product of the Cold War?. Intercontinental Books. ku. 117–. ISBN 978-0-9814258-5-6.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Roland Brown kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |