Rose Njilo
Rose Njilo (alizaliwa katika Wilaya ya Ngorongoro, mkoa wa Arusha, Januari 1988 [1]) ni mwanaharakati na mpigania haki za wanawake hasa wanaotoka katika jamii ya Kimasai; pia ni mkurugenzi [2] na mwanzilishi wa shirika la kutetea haki hizo la Mimutie Women Organization.
Rose Njilo | |
Amezaliwa | Januari 1988 Arusha |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | haki za wanawake |
Tuzo
haririMwaka 2020, Njilo alipata Tuzo ya Mwanamke bora anayepambana na ukatili wa kijinsia, tuzo ambayo ilitolewa na WILDAF kutokana na mchango wake katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii wa Kimasai.
Tuzo hizi hutolewa kila mwaka wakati wa maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zinazofanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Siasa
haririMbali na kupigania haki za wanawake katika jamii ya Wamasai, Rose amekuwa akihamasisha wanawake kushiriki katika ngazi za maamuzi ikiwemo kushiriki katika siasa. Mara nyingi amekuwa akijaribu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jimbo la Ngorongoro.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-11. Iliwekwa mnamo 2023-03-11.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/woman/chatting-gender-equality-for-sustainable-growth-3744354
Viungo vya Nje
haririMakala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |