Wilaya ya Ngorongoro

Wilaya ya Kaskazini, Tanzania

Wilaya ya Ngorongoro ni moja kati wilaya saba zinazounda mkoa wa Arusha nchini Tanzania yenye postikodi namba 23700. Ilikuwa sehemu ya wilaya ya Masai iliyojumuisha Monduli, Kiteto, Simanjiro na Ngorongoro kabla ya kugawanywa mwaka 1975 na kuongozwa na marehemu Lazaro Parkipuny kwa muda wa miaka 20.

Mahali pa Ngorongoro (kijani) katika mkoa wa Arusha.

Wilaya hii inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Monduli kwa upande wa Mashariki, Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini na mkoa wa Mara kwa upande wa Magharibi.

Wilaya hii ina historia ya pekee kwa kuwa ni sehemu yenye vivutio vingi. Eneo maarufu na linalojulikana sana ulimwenguni ni hifadhi ya Ngorongoro iliyopo ndani ya kasoko ya volkeno bwete (baridi) na kasoko hii iko katika wilaya hii. Pia mlima wenye volkeno hai ujulikanao kama Oldoinyo Le Ngai upo katika wilaya hii. Kwa maana hii sehemu kubwa ya wilaya hii imehifadhiwa: ni asilimia kama 60.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro ilihesabiwa kuwa 174,278. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 273,549 [1].

Kabila kuu katika wilaya ya Ngorongoro ni Wamaasai.

Misimbo ya posta katika wilaya hii huanza kwa tarakimu 237 (23701 - 23721).

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Ngorongoro - Mkoa wa Arusha - Tanzania  

Alailelai | Alaitolei | Arash | Digodigo | Enduleni | Engaresero | Enguserosambu | Eyasi | Kakesio | Kirangi | Maalon | Malambo | Misigiyo | Nainokanoka | Naiyobi | Ngoile | Ngorongoro | Olbalbal | Oldonyosambu | Oloipiri | Olorien/Magaiduru | Ololosokwan | Orgosorok | Pinyinyi | Piyaya | Sale | Samunge | Soitsambu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.