Mkoa wa Arusha
Mkoa wa Arusha ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 23000, na ni wa pili kwa utajiri nchini.
Mkoa wa Arusha Chimbuko la Binadamu |
|
Mahali pa Mkoa wa Arusha katika Tanzania | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 6 |
Mji mkuu | Arusha |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | John Mongella |
Eneo | |
- Jumla | 34,526 km² |
- Kavu | 33,809 km² |
- Maji | 707 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 2,356,255[1] |
Jina la watu | Arushan |
Msimbo wa posta | 23xxx |
Tovuti: http://www.arusha.go.tz/ |
Wakazi ni 2,356,255[2].
Eneo
haririEneo lake ni km za mraba 34,526 zikiwemo km² 707 za maji ya ndani.[3].
Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara.
Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini, Ngorongoro na Karatu.
Makao makuu yapo Arusha mjini.
Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (m 2,878) ni volkeno hai bado, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910.
Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu.
Uchumi
haririMkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu.
Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti.
Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Kati ya wakazi asili wa mkoa ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamasai.
Majimbo ya bunge
haririWakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Arumeru Magharibi: mbunge ni Noah Lembris (Chama Cha Mapinduzi)
- Arumeru Mashariki: mbunge ni Dkt. John D. Pallangyo (Chama Cha Mapinduzi)
- Arusha Mjini: mbunge ni Mrisho M. Gambo (Chama Cha Mapinduzi)
- Karatu: mbunge ni Daniel Awack (Chama Cha Mapinduzi)
- Longido: mbunge ni Dkt. Steven Lemomo Kiruswa (Chama Cha Mapinduzi)
- Monduli: mbunge ni Fredrick Lowassa (Chama Cha Mapinduzi)
- Ngorongoro: mbunge ni Emmanuel Ole shangai (Chama Cha Mapinduzi)
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/
- ↑ https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/
- ↑ Historia, tovuti rasmi ya mkoa wa Arusha
Viungo vya nje
hariri
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Arusha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |