Roskosmos
Roskosmos (rus. Роскосмос) ni jina la kifupi la shirika la serikali ya Urusi kwa shughuli za kiraia kwenye anga-nje. Jina kamili kwa Kirusi ni Государственная корпорация по космической деятельности (gosudarstvenaya korporatsiya po kosmocheskoi deyatelnosti "shirika ya kiserikali ya shughuli za angani").
Shirika hili lilianzishwa tarehe 1 Januari 2016 kwa amri ya rais Putin likachukua nafasi ya mamlaka ya kitangulizi yenye jina lilelile.[1][2]ROSKOSMOS iliyounganishwa na Shirika la Roketi na anga-nje (Объединенная ракетно-космическая корпорация, United Rocket and Space Corporation)iliyowahi kutengeneza vyombo vya anga.
Roskosmos mpya inahusika na miradi yote ya kiraia (tofauti na miradi ya kijeshi) ya Urusi kwenye anga. Makao makuu yapo Moscow na kituo cha kufunza wanaanga kipo kwenye "Mji wa nyota" (Swjosdny Gorodok). Kituo cha kurusha roketi kinapatikana Baikonur nchini Kazakhstan iliyokuwa kituo cha Umoja wa Kisovyeti.
Kwa ujumla shirika la Roskosmos linachukua nafasi ya taasisi mbalimbali zilizohusika zamani ya ukomunisti katika Umoja wa Kisovyeti kupanga, kutengeneza na kutoa roketi na vyombo vya angani kama vile Sputnik 1, Soyuz na MIR.
Wanaanga Warusi (zamani za Umoja wa Kisovyeti)
-
Yuri Gagarin, binadamu wa kwanza aliyefika kwenye anga la nje.
-
Mwanaanga Aleksei Leonov, mtu wa kwanza aliyetembea kwenye anga la nje kwa kutoka katika chombo mwaka 1965.
Marejeo
- ↑ Russian space agency gets replaced by state corporation — Kremlin Ilihifadhiwa 6 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine., TASS 2015-12-28, ikitazamiwa 2016-02-02
- ↑ Russian Space Follies, NASA Watch 2015-12-30, ikiangaliwa tar. 2016-02-02
Viungo vya Nje
- (Kirusi) Tovuti ya Roskosmos, kwa Kirusi na Kiingereza Ilihifadhiwa 9 Agosti 2013 kwenye Wayback Machine.
- RKA home page in English Ilihifadhiwa 26 Julai 2016 kwenye Wayback Machine.
- Russian Space Program
- The future of the Russian space program Ilihifadhiwa 12 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.. Infographics from RIA Novosti.