Rudi
"Rudi" ni jina la wimbo uliotolewa tarehe 1 Novemba 2017 na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Rich Mavoko. Wimbo umemshirikisha msanii wa muziki wa ragga kutoka nchini Nigeria, Patoranking. Huu ni wimbo wa pili kwa Patoranking kushirikiana na msanii kutoka katika ngome ya WCB. Awali alifanya na Diamond Platnumz katika Love You Die uliotoka 1 Septemba, 2017. Ambamo Diamond alikamia kisawasawa ushirikishwaji wake katika wimbo huo.[1]
“Rudi” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava la "Rudi"
| |||||
Single ya Rich Mavoko akiwa na Patoranking | |||||
Imetolewa | 1 Novemba, 2017 | ||||
Muundo | Upakuzi wa mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2017 | ||||
Aina | Bongo Flava, ragga | ||||
Urefu | 3:39 | ||||
Mtunzi | Rich Mavoko Patoranking | ||||
Mtayarishaji | Abby Daddy S2Kizzy | ||||
Mwenendo wa single za Rich Mavoko akiwa na Patoranking | |||||
|
Wimbo huu wa Rudi ni ushirikiano wa watayarishaji wawili mahiri Abby Daddy akiwa na S2Kizzy. Video ya wimbo huu imeongozwa na Mr. Moe Musa ambaye ndiye aliyeongoza kazi nyingine ya WCB kama vile Halellujah (2017) na Bum-Bum (2014). Wimbo ulitambulishwa kama sauti mnamo tarehe 25, Oktoba, 2017 na kuja kutolewa rasmi mnamo tarehe 1 Novemba, 2017.
Wimbo umeimbwa katika toni ya huzuni sana kupita kiasi. Huenda ukawa wimbo wa kwanza wa Mavoko kusikitika sana. Mwanzo hadi mwisho ameimba toni ya huzuni tu na si kupanda na kushuka kama jinsi anavyofanya katika nyimbo zake nyingi za awali. Anamlilia mpenzi wake aliyemwacha siku nyingi, anamwomba arudi katika pendo lao kwani ukimya wake una muumiza. Ubunifu zaidi katika wimbo huu na nyigine kadhaa zilizopita za wasanii wa Nigeria ni kutumia baadhi ya maneno ya Kiswahili katika uimbaji wao. Humu Patoranking kaimba kwa Kiswahili na kutia maneno kama:
"Nikiwa nawe mwenzako ndo napona,
Na nikilala usiku ndotoni nakuona,
Ukipata mafua me napa ka homa"[2]
Kufanya hivi, kunaongeza utangazaji wa Kiswahili kwa upande wa Afrika ya Magharibi. Lengo hasa ni kuisukuma Bongo Flava katika kiwango kingine kabisa. WCB ndio ngome pekee hadi sasa inayothubutu kusukuma muziki huu kimataifa. Awali alifanya A.Y kwa kumshirikisha Maurice Kirya katika wimbo wake wa Binadamu (2004) na Lady Jay Dee kuweni "Makini" alimshirikisha Titi. A.Y yeye aliyemshirikisha Sean Kingston kutoka Jamaica katika wimbo wake wa "Touch Me Touch Me" ambao Miss Triniti.
WCB imeazimia kuusukuma muziki huu wa Bongo Flava mbali zaidi. Hata video ya wimbo huu ilifanywa nchini Uingereza kama ilivyofanywa Halellujah.[3]
Huu ndio wimbo wa mwisho Rich Mavoko kutolewa chini ya lebo ya WCB. Baada ya gumzo kwa takriban miezi mitatu minong'ono ya chini kwa chini ya kwamba Rich katoka WCB.[4]
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Rudi katika wavuti ya DJ-Mwanga. "AUDIO | Rich Mavoko Ft. Patoranking - RUDI"
- ↑ Mashairi ya Rudi katika Lyrics Genius
- ↑ Rudi katika Bongo5.
- ↑ "Rich Mavoko ' aitosa' WCB", Mwananchi (kwa Kiingereza), 2018-07-26, iliwekwa mnamo 2018-08-03