Rukh-Shana Namuyimba

Mwandishi wa habari wa Uganda

Rukh-Shana Namuyimba ni raia wa Uganda aliyebobea katika tahasusi ya mawasiliano. Pia ni mwandishi wa habari, na mwanzilishi wa kampuni ya Xfinity Communications Ltd.

Mwanzoni alikuwa akifanya kazi katika kituo cha NTV Uganda, kabla ya kuelekea NBS Television.[1]

Maisha ya Awali na Elimu hariri

Rukh-Shana (amezaliwa Oktoba 17, 1978, Kampala) ni binti wa Meja mstaafu Al Hajji Badru Namuyimba, ambaye aliwahi kuwa rubani wa ndege katika kikosi cha anga wakati wa Idi Amin, na Hajat Jannet Namuyimba, mtumishi wa umma mstaafu. Familia yake ilikimbilia uhamishoni Nairobi, Kenya, miezi michache tu baada ya kuzaliwa. Waliishi Nairobi hadi alipokuwa na umri wa miaka 10. Aliporejea Uganda mwaka wa 1988, alijiunga na Shule ya Msingi ya Bwala Muslim Bweni huko Masaka. Alihudhuria King's College Budo kutoka 1991 hadi 1996 kwa elimu ya sekondari na A' Level.[2]

Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere mnamo 1997 hadi 2000, ambapo alipata Shahada ya Sanaa (BA), mawasiliano, fasihi na lugha ya Kiingereza.[2][3] mnamo mwaka 1997.[4]



Marejeo hariri

  1. BigEyeUg3 (2015-10-12). NBS TV officially unveils Rukh-Shana Namuyimba and Solomon Serwanjja, reveals why they were hired. (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-06-02. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
  2. 2.0 2.1 Rukh-Shana Namuyimba Opens Up on Breaking Ranks, Quest for Spiritual Eternity, and Upended Life Plans! (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-10-28. Iliwekwa mnamo 2023-10-28.
  3. Makerere University. Faculty of Arts. Makerere University. Faculty of Social Sciences. Makerere University College. Faculty of Arts. Makerere University College. Faculty of Social Sciences. (1967). Mawazo. Faculties of Arts and Social Sciences, Makerere University. OCLC 300956288. 
  4. The Inter-Institutional Media Challenge (en) (2016-12-04).
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rukh-Shana Namuyimba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.