Ryan Ackroyd

Mdukuzi


Ryan Ackroyd, almaarufu kama Kayla[1] na lolspoon, alikuwa mdukuzi wa aina ya kofia nyeusi, mmoja wa washirika wakuu wa kikundi cha udukuzi cha LulzSec[2][3] wakati wa siku ya 50 ya mashambulizi kutoka 6 Mei 2011 hadi 26 Juni 2011.[4] Wakati huo, Ackroyd alijulikana kama mdukuzi kwa jina lake "Kayla" na alikuwa amehusika na udukuzi wa mifumo mbalimbali ikiwemo ya kijeshi, ya kiserikali na katika mitandao maarufu zaidi ikiwemo mitandao ya Gawker mnamo Desemba 2010, HBGaryFederal in 2011, PBS, Sony, Infragard Atlanta, Fox Entertainment na mingineyo mingi.

Ryan Ackroyd
Amezaliwa Ryan Ackroyd
1 Januari 1988 (1988-01-01) (umri 36)
Iraq
Kazi yake Mdukuzi

Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, Ackroyd alisema waziwazi wakati wa mazungumzo na Lulzsec[5] kwamba anaamini wadukuzi wasiofahamika, wanaharakati wengine na wenye nia kama hiyo wanapaswa kukusanyika na kujaribu kufanya masuala ya udukuzi kihalali. Mnamo Desemba 2014, alitoa hotuba yake ya kwanza katika ukumbi wa hotuba wa Chuo cha Sheffield Hallam kwa zaidi ya wanafunzi 200, ambapo alizungumza juu ya Lulzsec na "siku zao 50 za lulz".

Kwenye akaunti yake ya Twitter, Ackroyd aliapa kusaidia usalama wa mifumo aliyowahi kudukua hapo awali, akisema kwamba "atasaidia kulinda na kutetea mifumo hiyo kwa matumaini ya kwamba tunaweza kujifunza kutoka kwa mwingine, endapo nitapewa nafasi ya kufanya hivyo". Aliongezea pia "Kwangu, haikuwa juu ya kuiba taarifa za watu, nilitaka tu kuwaonyesha watu jinsi mifumo yao ilivyokuwa hafifu katika usalama. Watu wanahitaji kurekebisha vitu vyao... Nilituma barua pepe nyingi kwa kampuni na hata mashirika ya serikali nikapuuzwa... Ndipo nilipogundua nilipaswa kuwaonyesha ni kwa nini wanapaswa kujilinda kabla ya kunisikiliza. Mimi ni kama Jiminy Cricket, wakati usiponisikiliza ningekugonga sana na mwavuli wangu mdogo ili ufanye jambo sahihi," alitania.

Historia

hariri

Inasemakana Ryan alikuwa na tatizo la low latent inhibition (LLI)[6] ndiyo maana alipenda na kutaka kujifunza jinsi kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa mwanajeshi mchanga ambaye alitumikia Iraq ambapo alijishughulisha maalum katika usalama wa mawasiliano na mifumo ya kijeshi.

Marejeo

hariri
  1. "Lulzsec hacker 'Kayla' pleads guilty to cyber crime in U.K." VentureBeat (kwa American English). 2013-04-09. Iliwekwa mnamo 2020-02-19.
  2. "The 6 men alleged to be LulzSec hackers include teenagers, female-impersonators, the unemployed", Christian Science Monitor, 2012-03-08, ISSN 0882-7729, iliwekwa mnamo 2020-02-19
  3. Charles Arthur, Ryan Gallagher (2011-06-24). "LulzSec IRC leak: the full record". the Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-02-19.
  4. "LulzSec's Top 3 Hacking Tools Deconstructed". Dark Reading (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-03. Iliwekwa mnamo 2020-02-19.
  5. "In conversation with former Anonymous and LulzSec hacktivists". Royal Court (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-02-19.
  6. http://www.lowlatentinhibition.org/what-is-lli/
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ryan Ackroyd kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.