Kiparara
(Elekezwa kutoka Rynchops)
Kiparara | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Viparara (au Ndege-msumeno) ni ndege wa bahari wa jenasi Rynchops, jenasi pekee ya familia Rynchopidae (Rhynchops na Rhynchopidae ni tahajia nyingine isio sahihi kwa mujibu wa uainishaji). Ndege hawa wanafanana na buabua lakini wana domo ambalo sehemu yake ya chini ni refu kuliko ile ya juu. Huruka kwa urefu mdogo juu ya maji wakiitia sehemu ya chini ya domo lao majini ili kuwakamata samaki wadogo. Jike huyataga mayai 3-6 kwa pwani za kanda za tropiki na za karibu na tropiki.
Spishi ya Afrika
hariri- Rynchops flavirostris, Kiparara wa Afrika (African Skimmer)
Spishi za mabara mengine
hariri- Rynchops albicollis (Indian Skimmer)
- Rynchops niger (Black Skimmer)
Picha
hariri-
Indian skimmer
-
Black skimmer