Sabasaba (maana)
ukarasa wa maana wa Wikimedia
Sabasaba (pia: Saba Saba) ni namna ya kutaja namba 77 au kifupi cha tarehe ya 7 Julai au siku ya saba kwenye mwezi wa saba.
Inataja mara nyingi
- Sikukuu ya Saba Saba ya kuundwa kwa chama cha TANU mwaka 1954 ni sikukuu ya umma katika nchi ya Tanzania; ilifutwa mwaka 1993 lakini kurudishwa kwa maana tofauti (angalia makala yenyewe)
- kifupi kwa maonyesho ya Dar es Salaam International Trade Fair katika Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania na eneo lake kwenye barabara ya Kilwa inayofanyika kila mwaka tarehe 7 Julai.
- jina la vitongoji, vijiji au kata kwa mfano
- jina la maeneo ndani ya miji mingi ya Tanzania ambako maonyesho yanafanyika
- Sabasaba nchini Kenya ni siku ambayo yanakumbukwa maandamano ya 7 Julai 1990 yaliyoleta mwisho wa utawala wa chama kimoja na chanzo cha demokrasia ya vyama vingi