Sabiki ya Hawaa (ar. & ing. Sabik, pia η Eta Ophiuchi, kifupi Eta Oph, η Oph) ni nyota angavu ya pili katika kundinyota ya Hawaa (Ophiuchus).

Sabiki ya Hawaa (Eta Ophiuchi, Sabik)
Sabiki ya Hawaa (Sabik) katika kundinyota yake ya Hawaa (Ophiuchus)
Kundinyota Hawaa (Ophiuchus)
Mwangaza unaonekana 2.43[1]
Kundi la spektra A : A1 IV B : A1 IV
Paralaksi (mas) 36.91
Umbali (miakanuru) 88
Masi M☉ A : 2.99 B : 3.47
Majina mbadala 35 Oph, BD–15°4467, GCTP 3895.00, Gl 656.1A/B, HD 155125, HIP 84012, HR 6378, SAO 160332, WDS J17104-1544AB

Nyota ya Sabiki ya Hawaa inayomaanisha ““mwenye kutangulia Hawaa (Ophiuchus)” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaoijua kama سابق sabiq kwa maana ya mtangulizi. [3].

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa tahajia ya "Sabik" [4].

Eta Ophiuchi ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu ya pili katika Hawaa ingawa Eta ni herufi ya saba katika Alfabeti ya Kigiriki. Hii ni mfano jinsi gani Bayer hakufuata mwangaza kikamilifu wakati wa kugawa majina ndani ya kundinyota.

Sabiki ya Hawaa ni nyota iliyo karibu kiasi ikiwa kwa umbali wa miakanuru takriban 88 kutoka Jua letu. Mwangaza unaoonekana ni mag 2.4. Kwa darubini nzuri inaonekana ni nyota maradufu inayofanywa na sehemu mbili η OphA na η OphB zinazofanana zikizunguka kitovu cha pamoja cha graviti. Kati yao kuna umbali wa vizio astronomia 33.5[5]. Jinsi zinavyozungukana imeleta hadi sasa matatizo kuhakikisha tabia zao.

Tanbihi

hariri
  1. Vipimo kufuatana na Docobo et al. (2007)
  2. ling. Knappert 1993
  3. Allen, Star-Names (1899), uk. 60
  4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  5. tazama Kaler, Sabik (Eta Ophiuchi)

Viungo vya Nje

hariri


Marejeo

hariri
  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
  • Docobo, J. A.; Ling, J. F. (April 2007), "Orbits and System Masses of 14 Visual Double Stars with Early-Type Components", The Astronomical Journal, 133 (4): 1209–1216 online hapa
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Ptolemy's Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sabiki ya Hawaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.