Kitara (silaha)
(Elekezwa kutoka Sabre)
Kitara (kwa Kiing. sabre au saber) ni silaha ya kukata. Ni aina ya upanga lakini nyepesi zaidi. Ubapa wake umepindika na kwa kawaida ni mwembamba zaidi. Una makali moja tu[1]. Zamani ilikuwa silaha ya askari farasi haswa.
Baadaye ilitumiwa pia kwa askari wa miguu. Tangu kupatikana kwa bunduki, ilitumiwa zaidi kama silaha ya mapambo ya afisa wa cheo cha juu jeshini.
Aina nyembamba za kitara hutumiwa leo kama vifaa vya riadha ambapo wanariadha wanapigana bila kujeruhiana (fencing).[2]
Marejeo
hariri- ↑ Marek Stachowski (2004). "The origin of the European word for sabre" (PDF). Studia Etymologica Cracoviensia. Krakow. 9.
- ↑ The Fencing Center, Sabre Fencing Ilihifadhiwa 17 Mei 2017 kwenye Wayback Machine. (accessed 16 Nov 2015)
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: