Saga koboa ni mchezo asilia wa watoto wa Afrika Mashariki.

Mchezo huu unashirikisha watoto wawili waliogeuziana migongo, kisha hupeana mikono kwa nyuma huku kila mmoja ameubana vizuri mkono wa mwenzake kwa mbele.

Hapo kwa zamu kila mmoja huanza kumnyanyua mwenzake akiimba “saga” na akimshusha chini wa pili huitikia “koboa”.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saga koboa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.