Samir Dey (10 Januari 195718 Novemba 2024) alikuwa mwanasiasa wa India kutoka chama cha Bharatiya Janata (BJP), Odisha ambaye aliwahi kuwa waziri wa Elimu ya Juu katika baraza la mawaziri la Naveen Patnaik kuanzia 2004-2009. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa Waziri wa Maendeleo ya miji katika baraza la kwanza la mawaziri la Naveen Patnaik kuanzia 2000-2004. Alikuwa mwakilishi wa Jiji la Cuttack mara tatu mfululizo 1995, 2000, 2004, katika Bunge la Jimbo la Odisha. Dey alifariki kutokana na maambukizi ya figo tarehe 18 Novemba 2024, akiwa na umri wa miaka 67. [1][2]

Samir Dey

Marejeo

hariri
  1. "Uphill task for Samir Dey, no cakewalk for Samantray". The New Indian Express. 2012-05-15.
  2. "Former minister lands in controversy". The New Indian Express. 2012-05-15.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Samir Dey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.