Sanamu za Memnon
Sanamu za Memnon (kwa Kiingereza: Colossi of Memnon) ni sanamu mbili kubwa za mawe za farao Amenhotep III, aliyetawala Misri ya zamani kipindi cha nasaba ya kumi na nane ya Misri. Tangu mwaka 1350 sanamu hizi zimesimama kwenye eneo la makaburi ya Theban yaliyopo mashariki mwa mto Naili.[1][2]
Maelezo
haririSanamu hizo pacha zinamwonesha farao Amenhotep III akiwa ameketi, huku mikono yake ikiwa imepumzika kwenye magoti yake na sura yake ikitazama mashariki kuelekea mtoni. Maumbo mengine mawili madogo yamechongwa kwa mbele kidogo sambamba na miguu yake: hawa ni mke wake Tiye na mama yakeMutemwiya. Paneli za pembeni inaonesha mmoja wapo kati ya miungu ya Misri ya zamani aitwaye Hapi.
Sanamu zote mbili zimeharibika kwa kiasi, huku sehemu za juu ya kiuno zikiwa ngumu kutambulika. Sanamu ya kaskazini ina kipande kimoja cha jiwe kubwa, lakini sanamu ya kaskazini ina ufa mrefu kwenye nusu ya chini huku sehemu za juu ya kiuno zikiwa na ngazi tano za mawe.[3] inaaminika kuwa hapo awali sanamu hizo mbili zilifanana kwa kila kitu, japokuwa michoro na sanaa zilizopamba zilitofautiana kidogo.
Kazi ya awali ya sanamu hizi ilikuwa ni kulinda lango la kuingilia kwenye hekalu lenye maiti ya farao Amenhotep wa tatu. Hekalu hilo ni jengo kubwa ambalo farao huyo alilijenga wakati wa uhai wake, ambapo aliabudiwa kama Mungu akiwa hai na baada ya kufariki dunia.
Picha
hariri-
Amenhotep III katika pozi la kuketi
-
Sanamu ya Memnon ya Magharibi au kusini
-
Sanamu ya Memnon ya Mashariki au Kaskazini.
-
Memnon
-
Picha Panorama ya Sanamu za Memnon
Marejeo
hariri- ↑ "Luxor, Egypt", BBC News. Retrieved on 2021-07-23. Archived from the original on 2013-04-19.
- ↑ Wilfong, T.; S. Sidebotham; J. Keenan; DARMC; R. Talbert; S. Gillies; T. Elliott; J. Becker. "Places: 786066 (Memnon Colossi)". Pleiades. Iliwekwa mnamo Machi 22, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Thebes and its five greater temples , by William de Wiveleslie Abney; published 1876 by Sampson, Low, Marston, Searle, & Rivington; archived at the University of Heidelberg
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sanamu za Memnon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |