Saratani ya mlango wa kizazi

Saratani ya mlango wa kizazi ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizomo ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi.[1]

Saratani ya mlango wa kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni:

  • Kutokwa na damu isiyo ya hedhi ukeni.
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
  • Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokoma hedhi.
  • Kutoka damu iliyochanganya na majimaji ya uke.
  • Matone ya damu kutoka au damu kutoka kipindi ambacho si cha hedhi.
  • Kutokwa na majimaji au uchafu ukeni wenye harufu mbaya wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu.
  • Kusikia maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni.
  • Kukojoa mkojo wenye damu.
  • Kupitisha mkono na haja kubwa ukeni na wakati mwingine,
  • Upungufu wa damu.

Shingo ya kizazi ni nini?

hariri

Shingo ya kizazi (‘cervix’) ni sehemu ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba.[2] Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo;

  • Kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi ili kupevusha yai
  • Kupitisha damu ya hedhi
  • Mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.[3]

Chanzo cha saratani ya kizazi husababishwa na aina ya virusi vinavyoitwa ‘Human Papilloma Virus’ (HPV), ambavyo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi.

Kuna tabia au hali hatarishi ambazo zinachangia mtu kupata saratani ya shingo ya kizazi, tabia/vitu hivyo ni pamoja na;

  • Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18).
  • Uvutaji wa sigara.
  • Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi.
  • Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
  • Kutokula mboga za majani na matunda.
  • Upungufu wa kinga mwilini.

Marejeo

hariri
  1. http://mpwapwadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/Saratani%20ya%20mlango%20wa%20kizazi.pdf
  2. Super User. "Saratani ya Shingo ya Kizazi (Cervical Cancer)". alexiamedical.co.tz (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-17. Iliwekwa mnamo 2020-09-16. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  3. "University of Dar es Salaam - University Health Centre". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2020-09-16.
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saratani ya mlango wa kizazi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.