Nzi-matunda Mdogo

(Elekezwa kutoka Scaptodrosophila)
Nzi-matunda mdogo
Nzi-matunda fumbatio-nyeusi (Drosophila melanogaster)
Nzi-matunda fumbatio-nyeusi (Drosophila melanogaster)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Familia ya juu: Ephydroidea
Familia: Drosophilidae
Róndani, 1856
Ngazi za chini

Nusufamilia 2:

Nzi-matunda wadogo ni nzi wa familia Drosophilidae katika oda Diptera wanaotaga mayai katika matunda, yale yaliyoanza kuoza ama yaliyopata madhara hasa, na katika maada nyingine ya mimea inayooza. Nzi-matunda wa familia Tephritidae ni wakubwa zaidi na hutaga mayai yao katika matunda yasiyooza.

Nzi hawa ni wadogo sana (mm 2-4) kwa kawaida lakini kuna spishi zilizo kubwa kuliko nzi-nyumbani (mm 15). Rangi yao ni njano, kahawianyekundu, kijivu au nyeusi na macho yao ni mekundu. Mara nyingi mabawa yana mabaka meusi.

Majike hutaga mayai katika maada inayooza ya mimea na kuvu, inayojumuisha matunda, maua, magome na viyoga. Mabuu ya spishi kadhaa, kama Drosophila suzukii, wanaweza kuharibu matunda kabla ya mavuno na kuletea wakulima hasara kubwa, lakini kwa kawaida nzi hao ni wasumbufu tu.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashriki

hariri