Sekunde ya tao

(Elekezwa kutoka Sekunde za tao)

Sekunde ya tao (ing. arc second) ni kipimo cha pembe. Inataja sehemu ya 3600 ya nyuzi moja.

Sekunde 60 za tao zinalingana na dakika moja ya tao. Dakika 60 za tao zinalingana na nyuzi moja. Nyuzi 360 ni sawa na duara kamili.

Kifupi chake ni arcsec au alama ya ".

Katika astronomia na upimaji wa Dunia pia kuna migawanyo midogo zaidi ya sekunde ya tao:

  • milisekunde ya tao au mas ni sehemu ya elfu moja (0.001″) ya sekunde moja ya tao
  • mikrosekunde ya tao au µas ni sehemu ya milioni moja ya sekunde ya tao.

Kipimo cha kawaida cha umbali katika astronomia (pamoja na kizio astronomia na mwakanuru) ni parsek inayofafanuliwa kuwa umbali kati ya Jua na gimba la angani linaoonekana kwa pembe ya paralaksi la sekunde moja ya tao (1 arcsecond).

Mifano

  • sekunde za tao 60 (=dakika 1 ya tao) zinalingana na pembe jinsi tunavyoona kiolwa chenye upana wa mita moja kwa umbali wa mita 3,438.
  • sekunde za tao 20 zinalingana na pembe jinsi tunavyoona kiolwa chenye upana wa sentimita moja kwa umbali wa mita 100.
  • milisekunde ya tao 1 inalingana takriban na pembe jinsi tunavyoona umbali wa mita 1.9 kwenye uso wa Mwezi.