Selemani Ndikumana
Sulemani Yamin Ndikumana (alizaliwa katika mji wa Bujumbura 18 Machi 1987} ni mchezaji wa mpira wa miguu anayeichezea klabu ya Lierse S.K. katika Ligi ya pili ya Ubelgiji na pia ni mchezaji katika Timu ya Taifa ya Burundi.
Selemani Ndikumana | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Sulemani Yamin Ndikumana | |
Tarehe ya kuzaliwa | 18 Machi 1987 | |
Mahala pa kuzaliwa | Bujumbura, Burundi | |
Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Lierse S.K. | |
Namba | 18 | |
Klabu za vijana | ||
Inter Star | ||
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2008 | Lierse S.K. | |
Timu ya taifa | ||
2006 | Burundi | |
* Magoli alioshinda |
Kutoka Norwei nakuelekea Ubelgiji
haririBwana Selemani alijiunga na klabu hiyo ya Lierse S.K. ya Ubelgiji kutoka kwenye klabu ya Molde FK ya Norwei mwaka 2008 mwezi Desemba baada ya klabu hiyo kuweka mkatabu bure na mchezaji huyo baada ya mkataba wa timu yake ya kabla ya Norwei kuisha,klabu hiyo ya Ubelgiji inategemea kuweza kogombea tiketi ya kujiunga katika ligi kuu ya Ubelgiji kwa msaa wa mchezaji huyo mzuri.
Kucheza kwake Ulaya
haririNdikumana Aliacha kuchezea klabu ya Inter Star klabu mashuhuri huko Burundi na alionekana mchezaji mzuri ndio klabu mashuhuri huko Tanzania ikatoa pesa nzuri ili aweze kuchezea klabu hiyo ambayo aliichezea kwa muda mrefu kidogo, baadae klabu ya Molde FK ya Norwei ikaomba kumchukua na alicheza baadhi ya mechi huko Norwei katika klabu hiyo, ila kijana mwenyewe alipiga kelele zaidi kutokana na baridi kali inayopatikana huko Norwei ndio akapata fursa yakujiunga na klabu ya Lierse S.K. huko ambayo ilimuomba nakutegemea anaweza toa mchango mkubwa katika kusaida kupatikina kwa magoli kwa wingi na alinunuliwa mwezi Desemba tar 8.
Jina lake Mashuhuri Burundi
haririJina lake mashuhuri huko Burundi ni Sele Drogba kutokana na uchezaji wake unaofanana na Drogba mwenyewe na katika wachezaji anaopenda duniani pia Drogba akiwemo.
Viungo vya nje
hariri- Kuhusu mchezaji katika klabu yake ya sasa ya Lierse S.K Ilihifadhiwa 25 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Video ya mchezaji katika klabu yake ya sasa katika kombe la Ubelgiji Ilihifadhiwa 18 Desemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Kuhusu mchezaji katika klabu yake ya kwanza ulaya Ilihifadhiwa 4 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Selemani kutia mkataba na klabu ya Ubelgiji ya Lierse Ilihifadhiwa 13 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- Baadhi ya picha na klabu yake mpya ya Lierse Ilihifadhiwa 23 Agosti 2011 kwenye Wayback Machine.
- Tornekrattet Profile Ilihifadhiwa 4 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Profile at National Football Teams
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Selemani Ndikumana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |