Seraphino Antao
Seraphino Antao (amezaliwa 30 Oktoba 1937) ni mwanariadha mstaafu kutoka Kenya. Alishinda katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya mwaka wa 1962, ikimfanya Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu katika shindano la kimataifa.[1]. Yeye ni wa asili ya Kiasia (Goan) kutoka jiji la Mombasa na alikuwa mkimbiaji wa mashindano ya masafa mafupi.
Kazi ya Mwanzo
haririSeraphino alikulia mitaa ya Ganjoni na Makupa jijini Mombasa. Nimwana wa Diogo Manuel na Anna Maria na ana ndugu sita. Akiwa Shule ya Upili ya Goan, alishiriki katika michezo lakini akiegemea riadha ya masafa mafupi.
Mnamo 1957 alivunja rekodi ya Kenya ya yadi 100 na 220[1].
Alishiriki katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 1958 kule Cardiff, Wales lakini hakuwa na mafanikio makubwa[1]. Miaka miwili baadaye alishiriki katika Mashindano ya Olimpiki ya 1960 jijini Rome, Italia ambapo alifika nusu fainali ya shindano la mita 100[2]. na mkondo wa pili katika shindano la mita 200[3].
Mafanikio ya Commonwealth na Hatima ya Kazi yake
haririKilele cha kazi yake kilikuwa wakati wa Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 1962 yaliyofanyika Perth, Australia. Hapa alishinda nishani ya dhahabu katika mbio za yadi 100 na 220. Pia alikuwa katika kikosi cha Kenya cha yadi 4X400 kupokezana vijiti kilichomaliza katika nafasi ya tano. Wengine katika kikosi hicho ni Wilson Kiprugut, Kimaru Songok na Peter Francis [4]. Mwaka huo huo alishinda dhahabu mbili (yadi 100 na 220) katika mashindano ya Ubinwa wa AAA nchini Uingereza, mashindano ambayo alikuwa ameshiriki mara zaidi ya moja[5]. Pia aliwahi kushinda nishani nyingi za Dhahabu katika Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati [6].
Kenya ilipata uhuru mnamo Desemba 1963 na Seraphino alikuwa mwanariadha wa Kwanza kuipeperusha bendera ya Kenya katika Mashindano ya Olimpiki ya 1964 jijini Tokyo, Japan[4], lakini alikuwa mgonjwa na hakutia for a ilivyokuwa ikitarajiwa. [7]. Alifika mkondo wa pili wa mita 200 kwa wanaume katika mashindano hayo[8] lakini akatolewa katika awamu ya mjujo katika shindano la mita 100 ref>Sports and Elections Statistics: Men 100m Olympic Games 1964 Tokyo (JPN)</ref>.
Baada ya Olimpiki
haririBaada ya Olimpiki alistaafu kutoka michezoni na kuhamia London, Uingereza ambapo anaishi hadi leo hii[1]. Mnamo 2003 alizuru nchini Kenya mara chache, akihudhuria sherehe za 50 za Kenya Amateur Athletics Association (Ambalo leeo hii huitwa ) [9].
Virejeleo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 Coastweek, 31 Januari 2003: Seraphino Antao - Super sprinter of the sixties
- ↑ Sports and Elections Statistics: Men 100m Olympic Games Rome 1960
- ↑ Sports and Elections Statistics: Men 200m Olympic Games Rome 1960
- ↑ 4.0 4.1 The Standard, 1 Februari 2003: Antao put Kenya on world map
- ↑ gbrathletics.com: AAA Championships
- ↑ gbrathletics.com: East and Central African Championships
- ↑ The Standard, 1 Februari 2003: Winning Two Gold in Perth Most Memorable
- ↑ Sports and Elections Statistics: Men 200m Olympic Games 1964 Tokyo (JPN)
- ↑ Daily Nation, 25 Januari 2003: Pioneer running hero back home