Serena de la Hey

Mchongaji sanamu wa Uingereza mzaliwa wa Kenya

Serena de la Hey (alizaliwa Eldoret, Kenya, 1967) ni Mkenya mwenye asili ya Kibritania, mchonga sanamu ambaye alikuwa akisafiri sana na makazi yake ya kudumu yalikuwa huko Somerset tangu miaka ya 1990. Alijulikana vyema kwa sanamu yenye urefu wa futi 40 kwenda juu Willow Man karibu na Bridgwater ambayo alimaliza majira ya vuli mwaka 2001.[1][2]

Serena de la Hey: The Willow Man (2001)

[[Jamii: Art and feminism]]

Wasifu hariri

Akiwa bado mdogo alitumia muda wake mwingi katika mashamba ya Australia. Baada ya kuhitimu chuo cha Falmouth Art College, aliweka makazi ya kudumu Somerset ambapo alianza kazi yake ya kwanza ya uchongaji wa sanamu kwa kutumia mierebi kutoka Somerset Levels.[1]

De la Hey alianza kutumia mierebi kuchongesha sanamu ya mfumo wa mtu mwaka 1992 ambapo alitengeneza takwimu endelevu za wicker ndani ya Nevada Desert.[3][4] [5] Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, amekuwa akitengeneza takwimu za wicker juu ya Watu na Wanyama kwenye studio yake iliyopo Stoke Gregory mkabala na Taunton. Anachukulia mierebi kama “njia rahisi zaidi ya kulifanyia kazi wazo”. Amezalisha takwimu kadhaa kwa wateja binafsi,nyingi zikiwa kama mapambo ya nyumbani na za bustani..[6]

Mnamo mwaka 2000, South West Arts walimlipa amtengeneze mtu kutokana na mierebi, sanamu ya urefu wa futi 40 kwenda juu ikikaribiana na M5 Motorway karibu na Bridgwater. Ilimchukua wiki nne kukamilisha uchongeshaji wa sanamu hiyo,kwa kutumia mierebi ya kawaida iliyotiwa nguvu na mnara wa chuma. Ilikamilika mwezi wa tisa 2000.[3]Mwezi wa tano 2001, vandals alichoma sanamu , akiacha mnara wa chuma pekee.[2]Nashukuru kwa kampeni ya kurejesha sanamu , mwezi wa kumi mwaka 2001, de la Hey alikamilisha awamu ya pili ,awamu hii alisuka waya wa chuma pamoja na mierebi. Kwa kuongezea , sanamu ililindwa na eneo kubwa lenye magugu.[7]Japokuwa mwanzoni iliundwa iweze kudumu kwa miaka mitatu tu , sanamu ya mtu wa mierebi imekuwa ikifanyiwa marekebisho mara kwa mara ndani ya mwaka na de la Hey na bado inaonekana vyema.[8]Marekebisho yamekuwa ya gharama sana ikimfanya de la Hey kufikiria kama sanamu hiyo angeweza kuichonga upya. [9]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Vere-Parr, Mary. "They're not corn dollies", 18 August 2001. Retrieved on 16 January 2018. 
  2. 2.0 2.1 Hesketh, Robert (14 January 2010). Somerset, Willow Woman, Serena De La Hey talks to Robert Hesketh. SomersetLife. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-01-25. Iliwekwa mnamo 16 January 2018.
  3. 3.0 3.1 "40ft sculpture unveiled in Somerset", BBC News, 26 September 2000. Retrieved on 16 January 2018. 
  4. 1992 Art Installations. Burning Man: The Culture Historical Archives (1992). Iliwekwa mnamo 16 January 2018.
  5. Template error: argument title is required. 
  6. Greer, Germaine. "Nice sculpture. Who made it?", 2 July 2007. Retrieved on 18 January 2018. 
  7. Willow man rises from ashes. BBC (19 October 2001). Iliwekwa mnamo 18 January 2018.
  8. "Repairs under way to Somerset's M5 Willow Man landmark", BBC News, 19 October 2015. Retrieved on 18 January 2018. 
  9. Willow Man may be removed because of high repair costs. ITV (12 October 2017). Iliwekwa mnamo 18 January 2018.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Serena de la Hey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.