Shahawa[1] ni kioevu cha mwili kilichoumbwa ili kubeba spermatozoo ndani yake. Mchanganyiko wa kioevu hicho na spermatozoo huitwa shahawa pia. Kinatolewa na tezi za shahawa na kwa kadiri ndogo zaidi na kibofushahawa ambazo zote mbili zimo katikati ya fupanyonga. Mchakato unaosababisha kutoka kwa shahawa kwenye kipenyo cha mrija wa mkojo unaitwa kumwaga. Kwa wanadamu kioevu cha shahawa kina vijenzi kadhaa badala ya spermatozoo: vimeng'enya, vinavyomeng'enya protini na molekuli nyingine, pamoja na fruktosi ni sehemu za kioevu vya shahawa ambazo zinasaidia spermatozoo kudumu na kuzipatia chombo ambamo zinaweza kusogea au "kuogelea". Kioevu hicho kimegeuka ili kutolewa ndani kabisa ya kuma, kwa hivyo spermatozoo zinaweza kupita kwenye uterasi na virijaova ili mojawapo iunde zigoti pamoja na yai.

Shahawa ya kibinadamu chini ya hadubini ikionyesha spermatozoo.
Shahawa ya kibinadamu kwenye sahani ya Petri

Tanbihi

hariri
  1. Kamusi nyingi zinasema kwamba neno hilo na manii ni visawe. Lakini Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia inapendelea manii kwa sperm na shahawa kwa semen. Sperm na semen ni tofauti.