Sharon Firisua
Sharon Firisua (amezaliwa 15 Disemba 1993) ni mwanariadha kutoka visiwa vya Solomon. Mnamo mwaka 2016 kwenye mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto alishindana katika mbio za mita 5000.[1] Mnamo mwaka 2020 kwenye mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto, alishindana kwenye marathon ya wanawake.[2]
Maisha ya kazi
haririMnamo 2013 alitajwa kuwa mwanariadha wa mwaka wa Visiwa vya Solomon[3]. Alianza mazoezi mwaka 2010, na katika michezo yake ya pili ya Pasifiki ya mwaka 2015 alichukua medali mbili za dhahabu kwa mita 5000 na mita 10,000[4] na nyingine katika mbio za nusu marathoni huko Port Moresby, Papua New Guinea.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-25. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
- ↑ "Athletics FIRISUA Sharon - Tokyo 2020 Olympics". olympics.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-02. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
- ↑ "Tokyo Olympics Results and Live Scores | NBC Olympics". results.nbcolympics.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
- ↑ "theislandsun.com". theislandsun.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-06. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.