Visiwa vya Solomon

Visiwa vya Solomon ni nchi ya visiwani ya Melanesia katika Bahari ya Pasifiki iliyoko mashariki kwa Papua Guinea Mpya.

Visiwa vya Solomon
Ramani ya Solomoni

Eneo lake ni visiwa karibu 1000, vyenye jumla ya km² 28,400 na wakazi 652,857, wengi wakiwa Wamelanesia (95.3%), wakiongea lugha 90. Lugha rasmi ni Kiingereza.

Kati yao 97.4% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Anglikana na Katoliki (19%).

Mji mkuu ni Honiara kwenye kisiwa cha Guadalcanal.

Historia hariri

Visiwa vimekaliwa tangu miaka elfu kadhaa na Wamelanesia.

Kuanzia karne ya 19 vilikuwa koloni la Ujerumani na la Uingereza.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mapigano makali kati ya Japani na Marekani yalitokea hapo.

Visiwa vilipata uhuru mwaka 1978.

 
Mashujaa wa visiwa vya Solomon wakiwa na silaha

Tazama pia hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.