Sherry Chen
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Sherry Chen; (alizaliwa Desemba 15, 1955) ni mwanamke mfanyabiashara na mbunge wa zamani wa Afrika Kusini .Chen alihamia Afrika Kusini mwaka 1981, alianza kufanya kazi kwenye kiwanda cha nguo, baadaye kama katibu wa Kiingereza kwenye kampuni ya biashara ya Wataiwan ambayo baadaye ilifilisika. Alifanya kazi zisizo za kawaida kwa muda kabla ya kupata kazi kwenye kampuni za kusafiri.
Chen baadaye alienselea kutafuta kampuni nne zilizofanikiwa zinazojihusisha kwenye mambo tofauti tofauti ya kibiashara. Chen alijihusisha na siasa mwaka 1994 kupitia mambo yake ya jumuiya Za kichina South Africa. Kwasababu ya kujikita kwenye biashara, hakuchukua ofisi mpaka alipofanikiwa kugombea Siti manispaa ya mji wa Johannesburg, akiipata mwaka 2000. Mwaka 2004, alichaguliwa kama mbunge. September 2010 Chen alijiuzulu nafasi yake ya bunge ili aendelee na biashara zake zaidi pamoja na kazi za ustawi wa jamii[1].
Tuzo
hariri- Randburg Business Person ya mwaka (1994)
- Gauteng Business Person ya mwaka (1994)
- 19 bora Global Chinese Businesswoman (2011)