Shilingi ya Tanzania
Shilingi ya Tanzania (kwa Kiingereza Tanzanian shilling; kifupi: TSh; code: TZS) ni fedha rasmi ya Tanzania. Imegawanyika katika senti (cents kwa Kiingereza) 100.
Shilingi ya Tanzania ilishika nafasi ya East African shilling tarehe 14 Juni 1966 at par.[1]
Kabla yake katika maeneo ya Tanzania ya sasa ziliwahi kutumika East African florin, East African rupee, Zanzibari rupee, Zanzibari riyal na German East African rupie.
Shilingi 100 zinaandikwa "100/=" au "100/-". Senti 50 zinaandikwa =/50 au -/50.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Linzmayer, Owen (2012). "Tanzania". The Banknote Book. San Francisco, CA: www.BanknoteNews.com.
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Bank of Tanzania page on circulating banknotes Archived 18 Januari 2013 at the Wayback Machine.