Shontelle

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Barbados

Shontelle Delia Layne (anajulikana kama Shontelle; amezaliwa 4 Oktoba 1985) [1] ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Barbados. Aliachia albamu yake ya kwanza inayoitwa Shontelligence mwaka 2008. Albamu yake ya pili, No gravity iliyotolewa mwaka 2010[2]. Nyimbo zake za "T-Shirt" na "Impossible" zilimpatia mafanikio kimataifa. Mnamo mwaka 2020 alitoa albamu inayoitwa "Remember Me".

Shontellle Mwaka 2010

Kazi hariri

2008–2009: Shontelligence:

Shontelle alianza kazi kwenye albamu yake ya kwanza studio mapema mwa mwaka 2008, na kuimaliza albamu hio ndani ya miezi sita. Jina la albamu hio alipewa na mhandisi wa albamu hiyo ambaye alitumia neno "shontelligence" kama utani baada ya Shontelle na wazalishaji wake kucheza mchezo ambao ulihusisha kutengeneza maneno kutoka kwa jina lake[3]. "T-Shirt" ni wimbo wa kwanza wa Shontelle, ulitolewa mnamo Julai 2008 na kushika nafasi ya thelathini na sita kwenye Billboard Hot 100 ya Marekani. Hata hivyo iliingia katika kumi bora katika chati ya nyimbo nchini Ubelgiji na Uingereza.[4]

Albamu ya kwanza ya Shontelle, Shontelligence, iliachiwa tarehe 18 Novemba 2008. Ilishika nafasi ya 115 katika chati za Billboard 200 za Marekani nakupata mauzo ya rekodi 6,200 katika wiki yake ya kwanza, na ilishika nafasi ya ishirini na nne kwenye chati ya Albamu za R&B/Hip-Hop[5]. Iliachiliwa tena mnamo tarehe 10 Machi 2009, na ilifanikiwa kuuza rekodi 30,000 nchini Marekani.

 
Shontelle akiwa anaimba mwaka 2008

Wimbo wake wa pili kwenye albamu, "Stuck with Each Other", akishirikiana na Akon, ilitolewa ,mnamo Februari 2009 nchini Marekani na kuachiliwa Mei 2009 nchini Uingereza. Wimbo huu ulisindwa kupata nafasi kwenye chati ya nyimbo za Marekani, lakini ilishika nafasi ya 23 nchini Uingereza[6] .Shontelle pia alishiriki katika ufunguzi wa ziara ya Beyoncé iliyoitwa " I Am .... World Tour" iliyofanyika kuanzia Mei mpaka Juni 2009.Shontelle pia alianza kuandika nyimbo kwa wasanii wengine huko Barbados[7].

2009–2010: No Gravity:

Shontelle albamu yake ya pili iliyoitwa "No Gravity" iliachiliwa Marekani tarehe 21 Septemba 2010[8]. Shontolle alisema albamu hiyo ipo kwenye majaribio kwakua alitaka kubadilisha sauti yake ya zamani kwenye rekodi[9]. Wakati jina la Albamu "No Gravity"linaashiria mantra, alisema kuwa ameweza kuzoea maisha yake ya kawaida na kazi zake na kumfanya ajiamini kuwa na uwezo wa kuendelea na chochote kitakacho mshikilia au kumrudisha nyuma[10]. Shontelle alishirikiana na Bruno Mars, Tony Kanal na Darkchild pamoja na wasanii wengine katika rekodi zilizopo kwenye albamu yake[11]. Katika wiki ya kwanza baada ya kuachiliwa kwa albamu ya "No Gravity" ilishikilia nafasi ya themanini na moja kwenye Billboard 200, ikiuza nakala 7,000[12]. Baadae Shontelle alitakiwa kushirikiana na Rihanna katika kuandika wimbo wa "Man Down" uliotoka albamu ya tano ya Rihanna iitwayo Loud (2010)[13][14].

Wimbo wake wa "Impossible" ambao ndo ulikua umeibeba albamu hio uliachiwa Februari 2010 kwaajili ya upakuaji kupitia mtandao lakini haikufanikiwa mpaka mwezi Mei 2010. Na umekua ndio wimbo wake uliofanikiwa zaidi mpaka sasahivi kwa kushika nafasi ya kumi na tatu 13, kwenye Billboard Hot 100. Wimbo wake wa pili kutoka kwa albamu hio, "Perfect Nightmare", ulitolewa mnamo Agosti 2010. Na wimbo wa "Say Hello to Goodbye" ulitumwa katika redio za pop mnamo 15 Machi 2011 ukiwa kama wimbo wa tatu.Nyimbo zote zilishindwa kuingia kwenye chati ya Hot 100, lakini zilishika nafasi katika chati ya nyimbo za Pop. "No Gravity" ilifanikiwa kuuza nakala 150, 000 nchini Marekani kufikia mwaka 2012.

2011-Mpaka Sasa:

Shontelle alicheza katika GUMBO @ The Canal Room huko New York City mnamo 15 Julai 2011, amabapo alitoa taarifa kuhusu albamu ya pili na ya tatu zitakazo tegemea kutoka. Pia ilifahamika kua aliondoka kutoka Universal Motown na kujiunga na Jamhuri ya Universal. Wimbo utakaobeba albamu ijayo ulifahamika kama "Reflection" na ulionyeshwa kwenye SoundCloud mnamo Septemba 2011. Nyimbo kwenye hio albamu zilitegemewa kuonyeshwa katika siku ya kuzaliwa ya Shontelle. Baadhi ya waliothibitishwa kua wamefanya kazi katika albamu hio walikua Rockwilder, Tony Kanal, na The Runners[15]. Mnamo Desemba 2012, Shontelle alithibitisha kuwa "Put Me on Blast" utakuwa wimbo uliobeba albamu yake ya tatu, na alikua tayari ameshachukua filamu za video za muziki huko Los Angeles. Albamu yake ya tatu ilipangwa kutoewa mwaka 2013, lakini haikuwa kutolewa na hamna tarege za baadae zilizotangazwa[16].

Mnamo Novemba 4, 2017, alitumbuiza na alikua ni jaji mgeni katika Miss Earth 2017 iliyofanyika Manila. Mnamo mwaka 2021, Shontelle alishirikiana na nyota katika filamu ya Amazon Prime Joseph, pia alisaini na Shakir Entertainment Management huko New York City katika runinga na filamu.

Mnamo 14 Machi 2020, Shontelle alitoa wimbo wake ulioitwa "Remember Me" kama utangulizi katika enzi yake mpya. Mnamo Aprili 9, 2021, Shontelle alishirikiana na Supasoaka pamoja kwenye wimbo ulioitwa "Let You Go" na Arpad.

Mnamo Oktoba 29, 2021, Shontelle alitoa wimbo wa utangulizi uliojulikana kama "Sanctify" kwaajili ya EP yake ijayo. Mnamo Januari 14, 2022, Shontelle alitoa wimbo "Be the One" ukiwa kama wimbo wa pili kutoka kwenye EP. Aliendelea kutoa nyimbo kama "No More", mnamo 14 Machi 2022. Mei 27, 2022 Shontelle alitoa EP yake inayoitwa "Boomerang" ambayo inajumuisha nyimbo mpya kama "Boomerang" na "Live It Up".

Marejeo hariri

  1. http://www.discogs.com/artist/Shontelle
  2. http://www.bluesandsoul.com/feature/388/shontelle_randbs_the_next_big_thing/
  3. http://www.bluesandsoul.com/feature/388/shontelle_randbs_the_next_big_thing/
  4. http://www.bluesandsoul.com/feature/388/shontelle_randbs_the_next_big_thing/
  5. https://www.billboard.com/artist/shontelle/chart-history/
  6. "ShontelleOnline.com | The Best Source for Shontelle Layne! | Shontelligence in Stores NOW!". web.archive.org. 2009-05-16. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-16. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  7. "Prom Ideas 2023 - Best Prom Party, Fashion, and Beauty Tips for Teen Girls". Seventeen (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  8. Shontelle, No Gravity (kwa English), SRP, iliwekwa mnamo 2024-04-19 
  9. "Shontelle 'plans new music direction'". Digital Spy (kwa en-GB). 2009-08-18. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  10. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-15. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  11. "Shontelle Talks New Album, Dream Collabo & Rihanna". ThisisRnB.com - New R&B Music, Artists, Playlists, Lyrics (kwa en-US). 2010-04-12. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  12. "Shontelle 'No Gravity' Debuts At... - That Grape Juice". thatgrapejuice.net. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  13. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-13. Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  14. Talking Shop: Shontelle (kwa en-GB), 2009-02-24, iliwekwa mnamo 2024-04-19 
  15. "Artists". Republic Records (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-04-19. 
  16. StarTrident.com is For Sale | BrandBucket