Shule ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma

Shule ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma ni moja kati ya shule kuu zinazopatika chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inayotoa masomo ya uandishi wa habari na mahusiano ya umma. Ilianzishwa rasmi tarehe 1 Aprili 2009.

Historia

hariri

Shule ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma imepata asili yake kutoka katika shule ya Uandishi wa Habari ya Tanzania, ambayo baadae ilikuja kujulikana kama, Taasisi ya Uandishi wa habari na mawasiliano ya Umma. Hiyo ilianza mwaka 1975 katika Hotel ya Zanzibar iliyopo Kisutu jijini Dar Es Salaam na baade kuhamia katika viunga vya Nyumba ya Luther karibu na Kanisa la Kilutheri, katika ukumbi wa mkutano wa mviringo katika jiji la Dar es Salaam

Shule ya uandishi wa habari ya Tanzania ilianzishwa rasmi chini ya sheria ya bunge namba 8, ya mwaka 1981, ilianza kwa kutoa stashahada kwa kipindi cha miaka miwili. Lakini kutokana na viwanja hivyo kuwa vidogo na kushindwa kutoshelza mahitaji ya kuanzishwa kwa stdio ya picha, ndipo ilipohamia katika viwanja vya Chuo cha kutoa mafunzo ya huduma za jamii karibu na kivukp cha Magogni hadi mwaka 1997

Katika mwaka huo huo, yaani mwaka 1997, Shule ya uandishi wa habari ya Tanzania ilihamia katika maeneo ya Salvation Army, mkabala na barabara ya Kilwa karibu na uwanja wa taifa, na Jeshi la Kujenga Taifa.

Shule ya uandishi wa habari ya Tanzania, ambapo waliendelea kutumia vyumba vya madarasa na vyumba vya makazi katika salvation Army, ambapo waliendelea kutoa stashahada. katika uandishi wa habari ambapo kwa wakati huo, chuo kilikuwa kimechukua wanafunzi thelathii (30) Mnano mwaka 1985, chuo kilihamia katika eneo la Shariff Shamba, ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama taasisi ya utamaduni ambayo ilihamia na kujenga afisi zake mpya katika wilaya ya Bagamoyo ambapo majengo ya Shariff Shamba yaliweza kukidhi haja za chuo hususani kwa upande wa ofisi za Utawala, madarasa na vyumba vya kulala wanafunzi kiasi cha wanafunzi 60 Shule ya uandishi wa habari ya Tanzania, ilipata vifaa vya studi ya redio, kamera na vifaa vingine kutoka katika shirika la nchini Denmark (DANIDA) kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 1997, chini ya usimamizi wa Proffesa Lisbert Rawn wa Shule ya uandishi wa habari ya Denmark, ambapo , wafanyakazi watatu waliweza kupata mafunzo kwa kiwango cha Uzamili katika Chuo Kikuu cha Cardiff chini ya udhamii wa shirika la DANIDA.

Wafanyakazi wengine watatu walipata mafunzo katika masuala ya Televisheni, redio za jamii na uzalishaji wa magazeti katika chuo cha Uandishi wa Habari cha Denmark kinachoitwa Arhus. Alikuwa Proffesa Lisbert Rawn,ambaye alichangia sana hadi kupatikana kwa viwanja vya mwisho vya shule ya uandishi wa habari ya Tanzania katika eneo la Mikocheni pembeni kidogo na barabara ya makaburini, mbali kidogo na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi hii ikiwa ni mnamo mwaka 1996.

Makazi ya kudumu

hariri

Juhudi hizi zilitambuliwa rasmi na raisi Benjamini William Mkapa, ambapo ndipo alipoamua kukabidhi rasmi viwanja vya kilichokuwa kiwanda cha filamu cha Tanzania kwa Shule ya Uandishi wa habari ya Tanzania. Shule ilianza kutoa Stashahada ya juu ya miaka mitatu, katika uandishi wa habari na stashahada ya uzamili katika Mawasiliano ya umma na mwaka mmoja wa cheti katika uandishi wa habari, na kuondosha stashahada ya miaka miwili. kkakkajnjamx,sncsajnclskcslknbcjushiojclsknsdihhjsiqjdskjbnkjcbs c

Wazo la kuwa sehemu ya chuo kikuu

hariri

Kufuatia kuongezeka kwa programu nyingi katika uandishi wa habari, shule sasa ikapata wazo la kuwa sehemu ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, wazo lililokuwepo tangu mwaka 1995, lakini hadi Mheshimiwa Mohammed Seif Khatibu, aliyekuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu, habari na sera, alipotangaza katika ufunguzi wa Baraza jipya la Uongozi wa chuo, tarehe 14/10/1999, kwamba kama kanuni, Serikali inaliunga mkono wazo la Shule ya Uandishi wa habari Tanzania kuwa sehemu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, na kuwa wazo hilo sasa si ndoto tena.

Alidokeza kuwa, kutokana na mabadiliko ya kijamii, kisisas na kiuchumi yanayotokea, yataihitaji shule ya Uandishi wa habari ya Tanzania kama taasisi yoyote ya kijamii, kujichunguza kama imekwisha kufikia lengo lauanzishwaji wake. Namnukuu " kama sio, ni wakati wa kubalika" Katika kuunga mkono , Shirika la Kimataifa la Kidachi (DANIDA) ambalo lilikuwa likijihusisha na shughuli mbalimbali katika kufundisha na na kutoa ushauri katika masuala mbalimbali ya shule hii, waliagiza watu wawili kwa ajili ya kuangalia mambo ya kishule na kitaalamu. Baada ya kupitia mtaala, vifaa vya kufanyia mafunz, wafanyakazi, na baada ya kufanya mahojiano na majadiliano na wahitimu mbalimbali wa shule ya Uandishi wab habari ya Tanzania na wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na washika dau. Washauri walipendekeza kuwa shule iwe chini ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Shule ya Uandishi wa habari iliamini kuwa iatapa mafanikio makubwa kama itakuwa sehemu ya taasisi kubwa kama chuo kikuu cha Dae Es Salaam. Shule itapata kuanzia nguvu kazi na vitendea kazi katika chuo cha Dar es Salaam na wakati katika wakati huo huo, kuimarisha nguvu yake katika kufanya tafiti mablimbali.

Shule pia ingeweza kusajili wanafunzi katika ushindani wa hali ya juu, ambapo matokeao yake yangesababisha kuongezeka kwa ujuzi wa wahitimu wanaohitimu katika shule hii. Lengo likiwa kuwa sehemu muhimu kwa kwa mafunzo ya uandishi wa habari na kufanya tafiti mbalimbali nchini.

Wazo au ndoto ambayo ingeweza kufikiwa kama tu, shule ingeweza kuwa chini au sehemu ya chuo kikubwa na chenye ufahari kama chuo kiuu cha Dar es Salaam.

Shule chini ya chuo kikuu cha Dar es Salaam

hariri

Kuanzishwa kwa Taasisi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma chini ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, ulikuwa chini ya Sheria ya Chuo kikuu namba 1970, sehemu ya 55 (1) (b), katika mkutano wake wa 56 uliofanyika tarehe 21/03.2002, ambapo kamati tendaji ya Baraza la chuo kikuu ilikubali pendekezo la kuiingiza shule ya Shule ya Uandishi wa habari ya Tanzania ndani ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, na kuifanya Taasisi ya uandishi wa habari na awasilino ya umma kuwepo, hii ikiwa ni tarehe 01/07/2003 baada ya raisi wa Jamuhuri ya Tanzania, mheshimiwa Benjamini William Mkapa kutaja sheria namba 8, ya mwaka 1981

Kazi za Taasisi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma

hariri

Kazi zake kubwa zilikuwa kama ifuatavyo.

-Kutoa vifaa kwa ajili ya mafunzo, kanuni na taratibu za uandishi wa habari, mawasiliano ya umma, afisa mahusiano na matangazo, na masomo mengine ya yanayolandana nauandishi wa habari kwa jinsi baraza litakavyo amua muda kwa muda.

-Kutoa mafunzo yanayoelekea kutambua utaalamu mkubwa na mdogo katika uandishi wa habari na masomo mengine yanayofanana na hayo.

-Kufanya tafiti katika nadharia, kuendesha na matatizo mbalimbali katika vyombo vya habari,taasisi na mafunzo ya uandishi wa habari

-Pia, kutoa ushauri kwa vyombo vya habari, mambo yahusianayo na vyombo vya habari nchini, kudhamini na kuwezesha majadiliano mbalimbali yanayohusiana na maswala ya habari, warsha, mikutano na semina.

Uongozi mbalimbali

hariri

Shule imepitia katika uongozi mbalimbali, wafuatao ni viongozi ambao wote walichaguliwa na Rais.

-Meshark Maganga.

-Samwilu Mwafisi.

-Gervaz Moshiro.

-Mwajabu Poss, (aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza)

Mshauri wa sasa wa wanafunzi, ambaye ni Profesa Bernadeta Killian, aliyechaguliwa tarehe 01/04/2009

Kuwa shule ya uandishi wa habari na mawasilino ya umma

hariri

Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kimefanya mabadiliko katika muundo wake, ambayo imefanya vitivo kuwa katika ngazi ya vyuo na shule. nahivyo iliyokuwa Taasisi ya Uandishi wa habari na mawasiliano ya umma kwa sasa imebadilishwa nakuwa Shule kuu ya Uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, chini ya chuo cha sanaa na sayansi ya jamii katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzai tarehe 1 Aprili 2009.

Idara za shule

hariri

Shule ina idara kuu tatu, yaani idara ya mawasiliano ya umma, idara ya uandishi wa habari na idara ya asifa mahusiano na matangazo. Shule ipo ianendeshwa na Mshauri wa wanafunzi na Mshauri msaidizi (masomo)

Malengo ya shule

hariri

Malengo ya shule ni kutoa mafunzo kwa wale wanaotaka kufanya kazi katika vyombo vya habari, ambavyo vina majukumu ya kutoa habari, kufundisha na kutoa mafunzo halisia kwa jamii ya Watanzania , Zaidi ya yote, shule inaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ambo tayari wapo katika vyombo va habari.

Masomo yanayofundishwa

hariri

Shule iantoa mafunzo yafuatayo -

1. Mafunzo ya muda mfupi ya cheti katika masomo ya muhimu( Kipindi kifupi fupi)

2. Cheti katika uandishi wa habri.

3. Shahada ya sanaa katika uandishi wa habari

4. Shahada ya sanaa katika Mawasiliano ya umma

5. Shahada ya sanaa katika mahusiano ya umma matangazo

6. Stashahada ya juu katika mawasiliano ya umma

Masomo yanayopangwa kutolewa

1. Uzamili katika sanaa ya Mawasiliano ya umma.

2. Udaktari katika Filosofia katika uandishi wa habari na mawasiliano ya umma

Vyombo vya habari vya shule

hariri

Katika kupata ujuzi wenye uhalisia, shule inamiliki vyombo vya habari kama vile , redio,, yeeni Mlimani Redio inayotangaza kupitia 106.5 fm, ambayo ina uwezo kufika umabli wa kilometa 300. Redio hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 25 Novemba 2001. Pia kuna televisheni ya Shule, yaani Mlimani televisheni ambayo kwa mara ya kwenza ilienda hewani mwezi wa pili mwaka 2009, na kuanza kutangaza rasmi tarehe 1 Juni 009 Pia, shule inamiki gazeti, linaloitwa The Hill Observer. ambalo nalo pia lilinatumia kwa ajili ya mafuzo kwa wanafunzi ili kuweza kupata ujuzi.

Viungo vya nje

hariri