Ali Hassan Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi (8 Mei 1925 - 29 Februari 2024) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.
Ali Hassan Mwinyi | |
Muda wa Utawala 5 November 1985 – 23 November 1995 | |
Waziri Mkuu | Joseph Sinde Warioba |
---|---|
mtangulizi | Julius Nyerere |
aliyemfuata | Benjamin Mkapa |
tarehe ya kuzaliwa | 8 Mei 1925 Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
ndoa | Siti Mwinyi |
dini | Uislamu |
Kabla ya hapo alikuwa Rais wa tatu wa Zanzibar baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi kwenye Januari 1984. Urais wa Zanzibar ulimfanya kuwa makamu wa rais wa Tanzania; hivyo aliteuliwa kugombea urais wa kitaifa wakati Julius Nyerere alipoamua kutogombea tena kwenye mwaka 1985. Mwinyi alichaguliwa akaacha cheo chake cha Zanzibar akawa rais wa Tanzania. Visiwani alifuatwa na Idris Abdul Wakil.
Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais.
Maisha
haririMwinyi alizaliwa Kivure kwenye Mkoa wa Pwani wa Tanzania bara lakini wazazi wake walihamia Unguja alipokuwa mdogo. Kuanzia mwaka 1933 alipokea elimu ya msingi na sekondari kwenye shule za Mangapwani na Dole Secondary School alikohitimu mwaka 1942. Baada ya masomo ya ualimu aliendelea kwenye Chuo Kikuu cha Durham nchini Uingereza [1].
Alianza kufundisha shuleni akaendelea kuwa mkuu wa chuo cha ualimu Unguja hadi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya elimu ya Zanzibar baada ya mapinduzi kwenye mwaka 1963. Mnamo 1970 alipewa uwaziri wa nchi katika ofisi ya rais akaendelea na vyeo mbalimbali katika serikali ya Zanzibar, pamoja na waziri wa afya, wa mambo ya ndani na wa utalii. Alihudumia pia miaka mitano kama balozi wa Tanzania nchini Misri. Mnamo Januari 1984 aliteuliwa kuwa rais wa Zanzibar baada ya mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi aliyelazimishwa kujiuzulu[2]. Katika nafasi kama rais wa Zanzibar alikuwa pia makamu wa rais wa muungano; katika uchaguzi wa 1985 aliteuliwa na CCM kuwa mgombea kwa nafasi ya raisi wa taifa akachaguliwa bila mpinzani katika mfumo wa chama kimoja.
Wakati wa urais wa kitaifa wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huria zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, Mwinyi alianzisha Tume ya Nyalali iliyopendekeza kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Wakati wa awamu yake kwenye mwaka 1995 ulitokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania.
Sera za soko huria za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam.
Heshima na Tuzo
haririNishani
haririNishani | Nchi | Mwaka | Ref | |
---|---|---|---|---|
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere | Tanzania | 2011 |
Shahada za Heshima
haririChuo Kikuu | Nchi | Shahada ya Uzamivu | Mwaka | Ref |
---|---|---|---|---|
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania | Tanzania | Daktari wa Barua | 2012 | [3] |
Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki | Kenya | Daktari wa Usimamizi wa Biashara | 2013 |
Tazama Pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Chancellor Hon. Dr. Ali Hassan Mwinyi, tovuti ya Kampala International University in Tanzania (KIUT), iliangaliwa Julai 2020
- ↑ Tanzanian Vice President Aboud Jumbe resigned Sunday from all his posts, tovuti ya UPI Archives Jan. 29, 1984, iliangaliwa Julai 2020
- ↑ "Why OUT awarded Mzee Ruksa a honorary degree". IPP Media. 24 Machi 2012. Iliwekwa mnamo 7 Februari 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Alitanguliwa na Mwinyi Aboud Jumbe |
Makamu wa Rais wa Tanzania 1984-1985 |
Akafuatiwa na Joseph Sinde Warioba |
Alitanguliwa na Julius Nyerere |
Rais wa Tanzania 1985-1995 |
Akafuatiwa na Benjamin Mkapa |