Sibusiso Zuma
Sibusiso Wiseman Zuma (amezaliwa Durban, KwaZulu-Natal, 23 Juni 1975) alikuwa mwanakandanda mtaalamu wa Afrika Kusini anayeichezea klabu ya kandanda ya Kideni Superliga inayoitwa FC Nordsjælland.
Sibusiso Zuma | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Tarehe ya kuzaliwa | ||
Mahala pa kuzaliwa | ||
* Magoli alioshinda |
Wasifu
haririZuma ilianza wasifi wake katika klabu za Afrika Kusini kama vile Mighty Pa, African Wanderers na Orlando Pirates. Mwezi Juni mwaka wa 2000, alijiunga na klabu ya Kideni ya FC København, ambapo alijiendeleza kama mchezaji. Aliisaidia klabu yake kushinda taji la ligi ya Kideni kwa mara yake ya pili na aliteuliwa kuingia katika “hall of fame” ya klabu kutokana na jitihada zake bora katika msimu wa 2004-05, na mwaka wa 2001 Zuma aliteuliwa katika nafasi ya 29 katika tuzo la mwanakandanda bora wa FIFA wa mwaka wa 2001. Baada ya miaka 5 ½ katika klabu ya FC København, Sibusiso Zuma aliuzwa kwa klabu ya Bundesliga, ambayo ni ya ligi ya Kijerumani, Arminia Bielefeld kwa kitita cha yuro milioni moja mnamo Julai 2005.
Mamelodi Sundowns
haririMnamo 21 Juni 2008 Sibusiso Zuma alisainiwa na klabu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns. Kisha aliachiliwa katika majira ya joto ya mwaka wa 2009 na mnamo Oktoba mwakwa wa 2009 alikuwa na kipindi cha majaribio na klabu ya FC Nordsjælland, [8] hatimaye kusainiwa na klabu hiyo.
FC Nordsjælland
haririMnamo 16 Oktoba alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Kideni ya FC Nordsjælland. Mnamo 8 Novemba 2009 Zuma alifunga bao lake la kwanza la FC Nordsjælland katika ushinid wa klabu wa 1-0 dhidi ya SønderjyskE.
Wasifu wa Kimataifa
haririYeye ameiwakilisha Afrika Kusini katika mechi 67. Aliicheza nchi yake katika Kombe la Dunia la FIFA la mwaka wa 2002. Zuma alikuwa nahodha wa timu ya kitaifa ya Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2006.
Historia
haririPia anajulikana kama "Zuma the Puma" kwa wafuasi wa klabu na "Puma" inaonekana kwa jesi lake badala ya "Zuma" katika mchezo wa komputa maarufu kama “video game” ijulikanayo kama Pro Evolution Soccer 2009 .
Tukio
haririMnamo 25 Juni 2007 iliripotiwa kuwa Zuma alikuwa amehusika katika tukio katika nchi yake ya nyumba ya Afrika Kusini. Baada ya ugomvi mkali kulikuwa na madai kwamba alitishia kuwapiga risasi kundi la watu katika sherehe katika sehemu ya Kokstad. Polisi wa mtaa walichunguza hali hiyo na Zuma alizuiwa kuondoka nchini kwa muda, lakini hakuna mashtaka yalitolewa.
Marejeo
hariri- [1] Archived 30 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- [2]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sibusiso Zuma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |