Kombe la Dunia la FIFA
Kombe la Dunia la FIFA ni mchuano wa kimataifa wa mchezo wa soka kwa wanaume. Kombe hilo hutambulika pia kama kombe la dunia la soka, kombe la dunia la mpira wa miguu au Kombe la Dunia tu.
Kombe hilo hushindaniwa na nchi wanachama wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA - Fédération Internationale de Football Association). Mashindano haya hutazamwa na watu wengi duniani kuliko mashindano yoyote yale. Mashindano ya mwaka 2002 watu wapatao bilioni 1.1 waliyatazama.
Baada ya hatua za mwanzo za kugombea kushiriki katika mchuano huu, nchi 32 hushiriki katika mchuano ambao hufanyika katika nchi inayoandaa/zinazoandaa mashindano hayo.
Hadi sasa ni nchi nane tu ambazo zimeweza kuchukua kombe hilo toka lilipoanza kushindaniwa hapo mwaka 1930. Mashindano hayo hufanyika kila baada ya miaka minne, ila mwaka 1942 na 1946 hakukuwa na Kombe la Dunia kutokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Brazili ndio nchi pekee ambayo imeweza kutwaa kombe hilo mara tano. Ujerumani na Italia zimelitwaa mara nne. Nchi nyingine ambazo zimewahi kulitwaa ni Uruguay, Argentina, Uingereza, Ufaransa na Hispania.
Ujerumani ndio nchi iliyoandaa Kombe la Dunia 2006 kati ya 9 Juni hadi 9 Julai. Bingwa wa kombe hilo, Brazili, ilitolewa kwenye mashindano hayo kwa kufungwa 1-0 na Ufaransa.
Kombe la Dunia 2010 lilifanyika katika bara la Afrika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Afrika Kusini.
Kombe la Dunia 2014 lilifanyika Brazili.
Kombe la Dunia 2018 linafanyika Russia.
Kombe la Dunia 2022 litafanyika Qatar.
Nchi washindiEdit
Nafasi | Nchi | Mshindi x |
Mwaka | Nafasi ya pili x |
Nafasi ya tatu x |
Nafasi ya nne x |
Fainali x |
Nusufainali x | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Brazil | 5 | 1958, 1962, 1970, 1994, 2002 | 2 | 2 | 2 | 6 | 8 | |
2 | Ujerumani | 4 | 1954, 1974, 1990, 2014 | 4 | 4 | 1 | 8 | 12 | |
3 | Italia | 4 | 1934, 1938, 1982, 2006 | 2 | 1 | 1 | 6 | 7 | |
4 | Argentina | 2 | 1978, 1986 | 3 | 5 | 4 | |||
5 | Uruguay | 2 | 1930, 1950 | 3 | 1 | 4 | |||
6 | Ufaransa | 1 | 1998 | 1 | 2 | 1 | 2 | 5 | |
7 | Uingereza | 1 | 1966 | 1 | 1 | 2 | |||
Hispania | 1 | 2010 | 1 | 1 | 1 | ||||
9 | Uholanzi | 3 | 1 | 1 | 3 | 3 | |||
10 | Chekoslovakia Ucheki |
2 | 2 | 2 | |||||
Hungaria | 2 | 2 | 2 | ||||||
12 | Uswidi | 1 | 2 | 1 | 1 | 3 | |||
13 | Poland | 2 | 1 | ||||||
14 | Austria | 1 | 1 | 2 | |||||
Ureno | 1 | 1 | 2 | ||||||
16 | Chile | 1 | 1 | ||||||
Kroatia | 1 | 1 | |||||||
Uturuki | 1 | 1 | |||||||
Marekani | 1 | 1 | |||||||
20 | Yugoslavia Serbia |
2 | 2 | ||||||
21 | Ubelgiji | 1 | 1 | ||||||
Bulgaria | 1 | 1 | |||||||
Umoja wa Kisovyeti Urusi |
1 | 1 | |||||||
Korea Kusini | 1 | 1 | |||||||
Kombe la Dunia ngazi ya klabuEdit
FinaliEdit
.[1]
Match was won during extra time | |||
Kigezo:Double dagger | Match was won on a penalty shoot-out |
Viungo vya njeEdit
- Tovuti ya FIFA Club World Cup
- Tovuti ya FIFA
- Tovuti ya Kombe la Dunia 2014
- Matokeo ya mechi za Kombe la Dunia toka 1930-2014
- Mashindano ya Kombe la Dunia yaliyopita
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kombe la Dunia la FIFA kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Santos Futebol Clube vs FC Barcelona. Fédération Internationale de Football Association (December 18, 2011). Iliwekwa mnamo March 4, 2013.
- ↑ 2.0 2.1 Corinthians – Vasco da Gama. Fédération Internationale de Football Association (January 14, 2000). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ 3.0 3.1 Futebol: Titulos (Portuguese). Sport Club Corinthians Paulista. Jalada kutoka ya awali juu ya March 4, 2013. Iliwekwa mnamo March 4, 2013.
- ↑ FIFA Club World Championship. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (January 10, 2013). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ Palmares: Primo Mondiale per Club FIFA – 2010/11 (Italian). Football Club Internazionale Milano S.p.A.. Iliwekwa mnamo March 4, 2013.
- ↑ Internazionale on top of the world. Fédération Internationale de Football Association (December 18, 2010). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ FIFA Club World Championship 2010. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (July 17, 2012). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ Cite error: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedFC Barcelona
- ↑ Santos humbled by brilliant Barcelona. 'Fédération Internationale de Football Association (December 18, 2011). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ FIFA Club World Championship 2011. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (July 17, 2012). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ Guerrero the hero as Corinthians crowned. Fédération Internationale de Football Association (December 16, 2012). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ FIFA Club World Championship 2012. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (January 10, 2013). Iliwekwa mnamo March 6, 2013.
- ↑ FIFA Klub-Weltmeisterschaft Sieger 2013 (German). Fußball-Club Bayern München e.V.. Iliwekwa mnamo January 27, 2014.
- ↑ FIFA Club World Championship 2013. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation (21 December 2013). Iliwekwa mnamo 21 December 2013.
Cite error: <ref>
tags exist for a group named "n", but no corresponding <references group="n"/>
tag was found, or a closing </ref>
is missing