Simba Wanyika ilikuwa bendi nchini Kenya iliyoundwa mwaka wa 1971 na ndugu kutoka Tanzania, Wilson Kinyonga na George Kinyonga. Bendi hii ilivunjika mwaka wa 1994. Simba Wanyika na bendi zingine mbili zilizotoka kwayo, Les Wanyika na Super Wanyika Stars, zilikuwa bendi mashuhuri sana nchini Kenya. Muziki wao uliotokana na sauti ya gitaa, ikiongozwa na mpiga gitaa wa Soukous, Dr Nico,ikichanganywa na maneno matamu ya muziki wa rumba na kuimbwa kwa Kiswahili. Simba wa nyika tafsiri yake kwa Kiingereza ni "Lions of the Savannah".

Wilson Kinyonga na George Kinyonga walianza muziki katika mji wao wa nyumbani wa Tanga nchini Tanzania walipojiunga na Jamhuri Jazz Band mwaka wa 1966. Walihamia Arusha mwaka wa 1970 na kuunda bendi ya Arusha Jazz na ndugu yao mwingine, William Kinyonga. Katika kipindi hiki, wanamuziki walikuwa wakisafiri watakavyo kati ya Kenya na Tanzania, na muziki wa Kenya ukashawishika sana na muziki wa rumba wa Tanzania. Mwaka wa 1971 ndugu hawa walihamia nchini Kenya na kuanzisha Simba Wanyika. Bendi ilitumbuiza katika vilabu vya usiku na baa mbalimbali katika jiji la Nairobi, nakupata wafuasi wengi mno, na katikati ya miaka ya 1970, walikuwa wanajulikana kote Kenya, kwa ajili ya nyimbo kama "Mwongele" na "Wana Wanyika".

Kutekelezwa kwa vikwazo baina ya mpaka wa Kenya-Tanzania ilisababisha watu kukua kwa muziki na kuelekea katika mtindo wa uliokuwa unajitokeza wa benga nchini Kenya. Simba Wanyika waliendelea kucheza rumba, na walikuwa bado maarufu wakati bendi ilipogawanyika katika miaka ya 1970 wakati mpiga gitaa Omar Shabini alichukua baadhi ya wanamuziki wake na kutengeneza Les Wanyika. Mwaka wa 1980, George Kinyonga pia alijiondoa katika Simba Wanyika, akachukua wanamuziki zaidi na kuunda bendi ya Orchestra Jobiso. Lakini baadaye alirudi Simba Wanyika huku bado akifanya miradi za upande na Jobiso. Simba Wanyika baadaye walibadilisha jina lao hadi "Simba Wanyika Original" ili kuzuia mkanganyiko na Les Wanyika na kundi lilojigawa kutoka kwao la Super Wanyika Stars.

Simba Wanyika ilirudia umaarufu wake katika katikati ya miaka ya 1980 wakitoa nyimbo zilizoptata umaarufu na baadaye kuzuru Ulaya mwaka wa 1989. Bendi ilivunjika mwaka wa 1994 lakini bendi kadhaa zilizotokana nayo bado ziko hai.

Angalia Pia

hariri

Viungo vya nje

hariri