Slothi
Slothi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Slothi koo-kahawia mwenye vidole vitatu
Bradypus variegatus | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 2, jenasi 2, spishi 6:
|
Slothi (kutoka Kiing.: sloth) au wavivu-miti ni mamalia wa ukubwa wastani wa familia Choloepodidae (slothi wenye vidole viwili) na Bradypodidae (slothi wenye vidole vitatu) wanaoainishwa katika spishi sita. Ni wana wa oda Pilosa na kwa hivyo huwa uhusiano na armadilo na walasisimizi walio na kucha sawa na zile za slothi. Spishi zinazopo hadu sasa huishi mitini mwa misitu mizito ya Amerika ya Kati na ya Kusini, na hujulikana kwa kusonga polepole, kwa hivyo walipewa jina la slothi ambalo kwa Kiingereza lina maana ya "mvivu", au kwa Kiswahili mvivu-miti.
Taksonomia na majina
haririNusuoda ya kitaksonomia ya slothi ni Folivora, wakati mwingine inaitwa Phyllophaga. Majina mawili yanamaanisha "mla-majani"; kutoka Kilatini na Kigiriki. Majina ya wanyama hawa yanayotumiwa na makabila ya Ekwado ni ritto, rit na ridette, ambayo humaanisha "kulala", "kula" na "mchafu" kutoka kabila ya Watagaeri wa Huaorani.
Spishi
hariri- Bradypus pygmaeus, Slothi Mdogo (Pygmy three-toed sloth)
- Bradypus torquatus, Slothi Manyoya-marefu (Maned three-toed sloth)
- Bradypus tridactylus, Slothi Koo-jeupe (Pale-throated three-toed sloth)
- Bradypus variegatus, Slothi Koo-kahawia (Brown-throated three-toed sloth)
- Choloepus didactylus, Slothi Kusi (Southern two-toed sloth)
- Choloepus hoffmanni, Slothi Kaskazi (Northern two-toed sloth)
Ekolojia
haririSlothi wanaainishwa kama wala-majani kwa sababu hula maua na majani kwa kawaida. Slothi wengine wenye vidole viwili hula wadudu, watambaazi wadogo na ndege. Majani wanayoyakula hayawatolei nishati nyingi, kwa hivyo, slothi wana utumbo mkubwa. Slothi hawawezi kuishi nje ya misitu ya mvua ya kitropiki ya Amerika ya Kusini na ya Kati, katika mazingira hayo slothi ni viumbe wanaoishi vizuri.
Picha
hariri-
Slothi mdogo
-
Slothi manyoya-marefu
-
Slothi koo-jeupe
-
Slothi kusi
-
Slothi kaskazi